Saturday, August 20, 2011

Wachanga shilingi 200,000 kupeleka kwa Binti Ndembo kumfichua mwalimu Athuman aliyepotea



WANANCHI wa Kata ya Msamala Kijiji  cha Msisima wamechangisha jumla ya shilingi 200,000 ili kuzipeleka kwa mganga wa jadi al maarufu kwa jina la Binti Ndembo aliyoko kilometa chache kutoka Mmanispaa ya Songea,ili aweze kumfichua mwalimu Athuman Athumani waliye potea mjini Songea.

Akizungumza na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi jina la shule halijulikani Bwana  Hamisi Hongo alisema mwalimu huyo alipotelea Mjini Songea mwezi Aprili mwaka huu akiwa na walimu wenzake kwenda kupokea mishahara yao na kufikia Guest House tofauti.

Walimu hao waliyefuatana naye mwalimu huyo walisema baada ya siku ya 4 walifika kwenye nyumba hiyo wa wegeni ambayo hawakuitaaja jina lake,waliambiwa mwalimu huyo hakuwepo katika chumba alicho chukua isipokuwa begi lake.

Mke wa mwalimu huyo Bibi Asha Jafari alipokwenda kwa Binti Ndembo aliambiwa kuwa mmewe yupo hai,hivyo kiasi cha fedha hizo kitalipwa kwa mganga huyo ili aende nyumbani kwa mwalimu huyo ili awatajie alikokuwa na jinsi ya kumrudisha.

Aidha kaka wa mwalimu huyo Bwana Saidi Athumani naye alipotea mwaka 2008 katika mazingira ya utata hadi habari hizi zinaletwa kwenye Blog hii hajulikani aliko.
( Source Fashen Milasi /Msisima Lusewa Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma )

No comments:

Post a Comment