Thursday, August 4, 2011

PROFESA JOSEPH MBELE AONGEA NA BAADHI YA WANACHAMA WA RUVUMA PRESS CLUB SERENGETI JIONI HII MJINI SONGEA BAADA YA KUTOKA MBAMBA - BAY

 Profesa Joseph Mbele wa Northfield Minnesota United States aliyevaa shati leusi na ukosi mweupe akiwa na baadhi ya wanachama wa Ruvuma Press Club katika ukumbi wa Serengeti katika Manispaa ya Songea jioni hii baada ya Prf. huyo kutokea Mbamba - Bay  ziwa Nyasa,kupata habari na pupata picha za mwambao mwa ziwa hilo.Wa kwanza kulia ni shemeji yake Prof.jina halikupatikana,wa pili mwenye sweeta yenye mistari ni Blogger Bw.Sikapundwa ( mwandishi wa habari ) wanne mwenye miwani ni Bw.Mwakanosya wa Nipashe.
 Dada Cresensia kapinga  mwenye gauni lekundu ni miongoni mwa waandishi wa habari wa club hiyo wakibadilishana nawaza na Prf.Mbele katika ukumbi wa serengeti mjini Songea.
 Ni picha ya pamoja na Prf,Mbele wakati akielezea jinsi wazazi wa Marekani wanavyo wasaidia watoto wao baada ya kutoka shuleni,iwapo watakwama katika somo ambalo wamepewa kazi ya kufanya nyumbani ( home work ) Hii inaonyesha jinsi wazazi wa -Tanzania wasivyo kuwa makini katika kufuatilia watoto wao wanaosoma na kile wanachojifunza kwa siku ile.
Profesa Mbele akizishangaa noti mpya za shilingi 2,000,5,000 na 10,000 za Tanzania  maana tangu noti hizo zianse kutumika ni mara yake ya kwanza kuzitumia baada ya kuingia nchini.Mwandishi wa Nipashe Bwana Gedion Mwakanosya aliyesimama akitoa maelezo mafupi kwa Profesa kuhusu noti hizo jioni hii katika ukumbi wa Serengeti Mjini Songea.

1 comment:

  1. Nilifurahi kukutana na kufahamiana nanyi na kujifunza hali halisi ya shughuli zenu katika kuuelimisha umma nchini mwetu na ulimwengu kwa ujumla. Mnafanya kazi ngumu, katika mazingira magumu, na mnastahili kuungwa mkono kwa hali na mali.

    ReplyDelete