Wednesday, August 17, 2011

TWIGA SI PANYA AMABAYE UNAWEZA UKAMFICHA NA KUMSAFIRISHA, INASHANGAZA TWIGA WETU WANASAFIRISHWA NA NDEGE UWANJA WA KIA ,KWENDA NJE HUKU TUNAONA.

Mchungaji Peter Simon Msigwa wa Iringa Mjini ( CHADEMA ) anashangazwa na aina ya usafirishaji wa wanyama wakubwa kama twiga kutolewa katika hifadhi hadi uwanja wa ndege wa Kia  kama wanayama wadogo kama panya asiyeweza kuonekana na kusafirishwa nje ya nchi.Hivyo ndiyo uwekezaji huo?,huo sio wizi wa wanyama wetu ?.

Aidha Mhe.Msigwa alisema kuwa lazima serikali ibadilishe mfumo uliyo kuwepo katika wizara ya maliasili na utalii uliyokuwepo.Maana waliyopewa dhamana wamepoteza uzalendo,watu waache kujinufaisha wenyewe badala ya kulinufaisha taifa.( Source Jambo Tanzania TBC )

1 comment:

  1. Jamani kama tutakwenda kwa mtindo huo, ina maana vizazi vyetu vitakuta jangwa, hakuna wanyama, makorongo ya machimbo....

    ReplyDelete