Thursday, August 11, 2011

MADAI MBALIMBALI YA WALIMU NI SHILINGI BILIONI 29 KWA MUJIBU WA CWT

 Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo akiongea na wakufunzi na walimu wa shule za mazoezi za sekondari na msingi katika usuluhisho wa mgogoro wa walukunzi na walimu na serikali juu ya madai yao ambayo ni madai yanayo daiwa na walimu wote nchini yenye  jumla ya shilingi bilioni 29.
 Mwakilishi wa wakufunzi na walimu katika chuo hicho Bwana Michael mahundi  alimweleza waziri kuwa wao wana madi saba,ambapo kila mmoja wao anamadai yake kulingana muda wa kuajiriwa.
 Aliyesimama ni mwalimu Simoni Sainyeye ambaye yeye alikuwa na msimamo mkali usiyo hata na nidhamu kwa naibu waziri,yeye hakupenda utaratibu uliyopangwa na Waziri wa kutaka kujua tatizo la kila mwalimu,yeye alichujua waziri kinda na Hundi zao za madai
.

 Ikabidi Makamu wa mkuu wa chuo hicho Bibi Triphonia Nchimbi kuwasihi walimu hao waliyojawa na jaziba ya kutaka kulipwa madai yao kwa serikali,lakini haikusaidia,Bali hekima na busara za naibu Waziri zikasaidia kupunguza munkali.

Baadaye Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Bibi Fidelia Lukuna akatoa karatasi yenya orodha ya majina ya baadhi ya walimu waliyohakikiwa na watalipwa fedha zao mwishoni mwa mwezi huu.Na wale ambao kulikuwa na makosa katika kuomba madai yao wataendelea kulipwa.
 Hawa ni baadhi ya wenye mgogoro na serikali wakiwakilisha walimu wote nchini wanye kuidai serikali.
 Ni walimu wenye madai tofauti tofauti lakini madai yenyewe ni pamoja na fedha za likizo,kupanda madaraja na kutokulipwa mapunjo ya mishahara .matbabu,uhamisho,kusoma,kuuguza na nyumba zilizohamwa lakini bado wanaendelea kukatwa mishahara yao.

Kaimu Mkurugenzi wa Ualimu Bibi Hellena Lihawa alisisitiza kuwa serikali inatambua madai yao,lakini ni wajibu wa kila muhusika mwajiriwa na mwajiri kufuata taratibu zilizowekwa kisheria katika kutatua na kudai haki mtumishi.Alisema madai ya walimu wote kwa katibu mkuu  wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi yanahakikiwa ili kila mmoja anaye dai alipwe stahili yake.

No comments:

Post a Comment