Sunday, August 14, 2011

Breaking News ! ! ! ! Mwanaharakati wa kupambana na vijana wanaotumia madawa ya kulevywa Dada Bupe amefanikiwa kutoa vijana kwenye vijiwe vya kutumia madawa

u
 Mwanaharakati Dada Bupe mwenye nguo nyeusi akiwa na binti ambaye hasikii lakini pia alikuwa mtumiaji wa madawa ya kulevywa yakiwemo bangi,unga, sasa kwa ushauri wa Dada Bupe binti huyo sasa amekuwa mjasilia mali katika standi ya mabasi Msamvu Morogoro.
 Huyo kijana sasa amerudi katika hali ya kawaida,katika jamii kutoka kwenye utumiaji wa madawa ya kulevywa na sasa anafanya kazi ya kupiga debe kwenye mabasi Msamvu Morogoro standi.
 Madawa ya kulevya hayachagui sura umbo elimu au mjinga,huyo bwana alikuwa akitumia unga,bangi na kujidunga sindano sasa baada ya ushauri wa dada Bupe na kushuhudia kwa macho yake mwenzake aliye nusa unga kugongwa na gari lililo msababishia kifo.naye aliogopa kutumia madawa nahuyaacha hadi sasa.
Rasta ni kawaida yao kuvuta bangi lakini huyo kayaacha madawa sasa anafanya shughuli zake Msamvu Morogoro.watumiaji madawa hawa majina yao hayakuweza kupatikana hapo Msamvu standi ya Morogoro.

No comments:

Post a Comment