Thursday, August 18, 2011

MKURUGENZI WA MALIASILI NA UTALII ASIMAMISHWA KAZI NA KULIPWA MSHAHARA NA WENZAKE WAWILI

 Waziri wa maliasili na utalii Mhe.Ezekiel Maige aliliambia Bunge leo kuwa Mkurugenzi wa Maliasili na Utalii Bw.Obed Mbangwa na wasaidizi wake wawili wamesimamishwa kazi leo tarehe 18/8/2011 kutokana na maombi ya baadhi ya wabunge kwa serikali kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo wakati uchunguzi unaendele kufanyika wa utoroshwaji wa wanyama,utoaji wa vibali kiholela.
 Mhe.Maige asisitiza kuwa migogoro ya mipaka katika hifadhi na utaratibu wa kutolewa kwa vitalu vya uwindaji itashughulikiwa.
Wabunge wamekuwa wakitaka kuwa huduma zinazotolewa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro iangaliwe upya.

No comments:

Post a Comment