Friday, August 12, 2011

NAUNGANA NA MHESHIMIWA ANNE MAKINDA SIPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA WABUNGE WOTE KUWA KITU KIMOJA

 Sipika wa Bunge Mhe Anne Makinda naungana naye pale alipowajulisha kile alichojifunza nchini Malawi kwenye mkutano wa wabunge,kuwa wabunge wakiwa ndani au nje ya bunge wanakuwa kitu kimoja nacho ni kutetea maslahi ya mwananchi na maendeleo ya taifa.'unapotetea hoja siyo unatetea hoja ya CCM,CHADEMA ama CUF bali ni hoja ya nchi.'Alisema Mhe.Makinda.alisema watuwakiwaona wabunge wa vyama tofauti  wakiongea wanashangaa kwanini wanaongea pamoja,kwani kuwa vyama tofauti uadui?
 Mheshimiwa Joseph Mbilinyi alisema serikali iwawezeshe vijana wanao andaa muziki kwani muziki ni ajira kwa vijana.wakati akichangia Wizara ya Habari,Utamaduni na Vijana leo siku ya pili ya bajeti ya Wizara hiyo.
 Wabunge wengi leo walizungumzia umuhimu wa kuinzi lugha ya kiswahili,lugha ya kiswahili ndiyo inayoeleza uzalendo wa mtanzania.,utawakuta watanzania 50 na mzungu mmoja utakuta mtu anavyo jikanyaga kuongea kiingereza asicho kielewa vizuri,walau naye aonekane yupo,kwanini mzungu huyo awe na mkalimani.
 Mheshiniwa Jenista Mhagama Mbunge wa Peramiho ,pia ni mwenye kiti wa kamati ya Wizara hiyo,anasisitiza kuwa asilimia 45 ni watoto wa umri wa mwaka mmoja hadi 15 na asilimia 45 nyingine vijana ambao wanashinda kwenye vijiwe visivyo na tija,serikali iwawezeshe hao katika sanaa na michezo ili wajiajiri.
Baadhi ya waandishi wa habari wanaharibu lugha ya kiswahili,wanapoandika habari zao,pia kuwa na sheria zinazo mbana mwandishi,hata akiandika vitu vya uchochezi aweze kuchukuliwa hatua,na wenye vyombo vya habari wawalipe waandishi wao fedha za kutosha ili kuondo tabia ya kuwanunua waandishi kuandika kile atakacho ambiwa.

No comments:

Post a Comment