Monday, August 15, 2011

BREAKING NEWS LEO BUNGENI KULIPENDEZA KWELI PALE WALIPO HOJI HATI MILIKI YA KIWANJA IWEJE ICHUKUE MIAKA NANE? NA YA CHAP CHAP SIKU MOJA AU MBILI? NA UGONJWA HUO UPO SDA DODOMA

 Mheshimiwa Hassan Zungu alisema kuwaondoa wakazi wa Jangwani ni kuwanyanyasa,kuwa pale hawakupenda ila hali yao ya kipato,alisema wako pale si kutaka utajiri bali ni kuwasomesha watoto wao.
 Waheshimiwa wabunge hao walikuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Ukweli wizara hiyo kuna ujanja ujanja unafanyika hasa katika upataji wa ofa na hati utazungushwa sijui ili ukate tamaa.
o
 Ukweli inawaathiri sana watu wasio na kipato kwa ajiri ya kununulia haki yako,masikini pesa yaziada ya kutoa ili upate ofa au hati itatoka wapi.Cha ajabu wanaohusika wanasikia na kilio cha wabunge ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi wanavyotetea.
 kila mmoja alichangia kutokana na hali anavyoiona na mapungufu ya wizara hiyo
 Mbunge wa Mtwara Mikindani anasema ili manispaa hiyo iwe ni lazima kata za Ziwani na Namayanga za Mtwara vijijini zipelekwe Mjini anauliza kigugumizi kiko wapo kwa serikali,alisema Mikindani ni Mji wa Kihistoria
Mbunge wa Kigamboni Dar es salaam anauliza hatima ya wakazi wa kigamboni iko wapi,wapo wananchi wenye uwezo wanaweza kuwekeza,na wale wenye uwezo mdogo wawe wabia na wawekezaji watakao wekeza kigamboni.

No comments:

Post a Comment