Bibi Erika Kaziulaya anayewatunza watoto yatima ( Orphans ) Kijiji cha Hanga kati wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma anawatunza watoto hao na kuwasomesha shule za msingi,sekondari hadi chuo kikuu,ameelemewa baada ya kuishiwa fedha ( fund )
Mama huyu ni shuhuda wa kijiji hicho anacho lelea watoto hao yatima Bibi kazi Ulaya
Bibi kazi Ulaya
Baadhi ya wanafunzi ( watoto yatima ) ambao Bibi kazi ulaya anawalea na kuwasomesha
Mwenye kiti wa kijiji hicho cha Hanga kati akimweleza ripota aliyetembelea kituo hicho cha kulelea watoto yatima cha Bibi Kazi Ulaya Hanga kati.Anasema kama Bibi kazi Ualaya amezidiwa kwa kukosa fedha za kuwalea watoto hao na kuwasomesha.hivyo anaiomba serikali kupitia wizara ya Maendeleo,wafadhili mbali mbali,wazazi na walezi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kumsaidia Bibi huyo Mjane aliyejitolea kwa nguvu zake kuwakusanya watoto yatima kuwalea na kuwasomesha hadi chuo kikuu.
AITWA OMBA OMBA BIBI ERIKA KAZI
ULYA BAADA KUELEMEWA NA MZIGO WA KUWALEA WATOTO YATIMA NA KUWASOMESHA KWA GHARAMA ZAKE
WENYEWE
Bibi Erika Kaziulaya ni mstaafu wa
chuoa cha ualimu Songea ambapo alifanya kazi kwa miaka 33,hatimaye akaitwa na
Mungu kuwa mlezi wa watoto yatima kijiji cha Hanga kati wilaya ya Nantumbo mkoa
wa Ruvuma.
Bibi kaziulaya analeya watoto yatima waliyofiwa na
wazazi wao,kwa mara yakwanza watoto hao
wakiwapeleka katika nyumba yake yakuwalea,wanakataa na kuogopa kwa kuwa labda
wametokea kwenye mazingirz ya kunyanyasika na kufanyiwa ukatili,lakini baada ya
muda wanazoea.
Bibi Kaziulaya aliyefiwa na Mumewe anawalea watoto
hao na kuwa somesha ambapo kati yao
mmoja anasoma chuo kikuu cha Tumaini mwaka wa kwanza na wengine 20 wanasoma sekondari
na seminari na anawagharimia mwenyewe kwa fedha za kinua mgongo ambazo sasa
zimemalizika.
Alisema kuna wengine wanasoma shule za msingi.Alisema
kuna kundi lingine walio maliza sekondari na wakashindwa katika mitihani yao ya taifa,hawa
anawafundisha ushonaji.
Anasema amenunuvyerehani na mwalimu mmoja
anawafundisha hapo tanyumbani kwa miaka miwili ( 2 ) baadaye wataenda kusoma
tena Hanga kwa miaka mingie miwili ( 2 ) ambapo watafanya mitihani ya VETA
kisha watajiajiri wenyewe.
Aidha Bibi Kaziulaya anaiomba serikali imlipe kinua
mgongo alichofundisha kwa miezi 9 ili aweze kuwalipia ada baadhi ya watoto hao
yatima wanaosoma sekondari na seminari na matumizi kwa huyo wa chuo kikuu.
‘Any body can
assist Mrs. Kaziulaya anything which you
think it help her in supporting those Orphans in school fees, food, soap,
sugar, vegetable anywhere you are please help this women engaged in orphans
help without enough fund using her won
source of income.’
Ukweli mama huyo anaomba msaada waina yoyote,ikiwa
fedha,chakula ,maji,sabuni,nguo,matandiko,madawa,vitanda.kutoka kwa
serikali,wazazi na walezi na wafadhili wa ndani na nje.mawasiliani kupitia TBC Kanda ya Ziwa Nyasa,Blog hii kwa e-
mail christiansikapundwa@yahoo.com
au +225756 -282369. ili kuwasiliana na Bibi Kaziulaya.
Ni moyo wa pekee kulea watoto wa watu ambao hana
mahusiano nao kiudugu wala hana mfadhili yeyote anayemsaidia.kwa hiyo kutoa ni
moyo humsaidii Bibi huyo,bali ni kuwasaidia watoto hawa waliyopoteza wazazi
wao.
No comments:
Post a Comment