Waandishi hao wa habari mjini hapa wamekuwa na faraja kubwa kukutana na Profesa Mbele ana kwa ana kwani Profesa huyo ni mara yao ya kwanza kukuta,ila kwenye mtandao wa Blog,hivyo wamepata chakula cha jioni kiitwacho mchemsho wa kuku,ndizi,nyanya chungu na njegere,lakini kwa Profesa hana matatizo na vyakula vyetu kwani yeye ni mzaliwa wa mkoa huu wa Ruvuma Wilaya ya Mbinga Matengo ( Litembo )
Hapa Profesa Mbele kabla ya wanahabari kuwasili katika ukumbi wa Serengeti Mjini hapa jioni hii ya tarehe 4/8/2011
Waandishi wa habari nao wanamambo wametaka kujua wasomi wa Marekani wa elimu ya juu ni sawa na wasomi wa elimu ya juu nchini Tanzania? Profesa aliwaambia kuwa wasomi wa Marekani wanasoma masomo mengi akatolea mfano kama mwanafunzi anasomea lugha huyo atasoma masomo mengi ili awe na ufahamu mpana katika elimu yake.Tofauti na elimu ya juu nchini kwetu.
Profesa Mbele anakwenda Dar es salaam kesho kupokea wanafunzi wake wanao fika kwenye ziara ya mafunzo,atakuwepo nao hadi tarehe 5/9/2011 kwa shughuli hiyo tu.Prof.anazichunguza noti mpya za Tanzania.
Inapendeza kukutana wanamtandao wa blog hata siku moja hamjawahi kulkutana ila kwenye mtandao.atakapo kuwepo Iringa atapenda kukutana na Mzee wa matukio,Blogger wa Iringa,na wa Mbeya.Aliyosimama naye Profesa Mbele mwenye shati leusi na ukosi mweupe ni baadhi ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma wakibadilishana mawazo na mgeni wao.
No comments:
Post a Comment