Dkt Ashibu Rozi Migiro Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa akiongea kabla ya kuzindua Ripoti ya Utafiti wa Ukatili dhidi ya mtoto Jijini Dar es salaam nchini Tanzania.
Mheshimiwa sophia Simba Mbunge akimkaribisha naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt Asha Rozi Migiro Jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa ukatili dhidi ya mtoto Jijini Dar es salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Dkt Asha Rozi Migiro alisema hayo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya
utafiti wa ukatili zidi ya watoto,Jijini Dar
es salaam.
Dkt.Migiro alisema nusu ya
wanzania ni watoto kama watafanyiwa ukatili
watoto watakuwa hawamwamini mtu kwa kujua ni mkatili,na kuwa na taifa la watu
wakatili hapo baadaye.
Alisema uzinduzi wa utafiti juu
ya ukatili kwa watoto kumeandika historia Afrika kwa serikali ya Tanzania kuridhia
utafiti huu kufanyika.Alisema watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili
mbalimbali.
Alivitaja ingawa si vyote kuwa ni
pamoja na kupigwa,kubakwa na kunajisiwa,kubebeshwa mizigo,kufanywa kazi kwenye
migodi kupewa mamba wakiwa na umri mdogo.
Aidha alisema Umoja wa Mataifa
unianza utafiti huu wa ukatili zidi ya watoto mwaka 1990 na Tanzania
ikaridhia kufanya utafiti na kupata ripotia,ambapo leoumezinduliwa na Dkt Asha
Rozi Migiro.
Alisema ripoti ya utafiti huu
imeonyesha kuna mambo mengi ambayo watoto wanafanyiwa ukatili,ubakaji na
unajisi unaweza kumpatia mwathirika magonjwa yakiwemo ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wenyewe na
magonjwa ya zinaa.
Alisema taasisi za kidini na
vyombo vya sheria vikiungana kumsaidia motto dhidi ya ukatili vitendo hivyo vitapungua,wazazi,mahakama
na polisi wakiwa na mshikamano wa kutosha mototo ataweza kuishi kwa amani kwa
kuwa anajua atalindwa na kuwa huru kujieleza pale apatapo matatizo.
No comments:
Post a Comment