Sunday, August 7, 2011

SERIKALI KUKARABATI VYUO VINNE VYA UALIMU VYENYE MIUNDOMBINU CHAKAVU

 Majengo ya chuo cha ualimu songea ambacho miundombinu yake imechakaa ikiwemo mifumo ya maji safa na maji taka, na vyoo vyake si safi kwa sababu ya ukosefu wa maji ya kutosha.
 Jengo la ukumbi wa mikutano na mbele ni jengo la maabara ya sayansi ambapo miundombinu ya maabara hiyo ni chakavu.
 Jengo la utawala na mbele yako ni jengo la madarasa pamoja na chumba cha computer science kwa ajili ya masomo ya TEHAMA.
 madarasa ya chuo hicho ambacho wakufunzi wake walikuwa na mgogoro na serikali toka tarehe 27 Julai mwaka huu hadi jana alipofika Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo kusuluhisha mgogoro na kesho wakufunzi hao wataanza kazi au kuingia madarasani


Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo akiwasalimia wanachuo wa chu hicho mara baada ya kuwasili chuoni hapo hapo jana.
Naibu waziri huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali imepanga fedha kwa ajili ya kukarabati vyuovinne vya ualimu nchini ambavyo miundombinu yake imechakaa.
Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na chuo cha ualimu Songea,Mpuguso,Vikindu na Ndala.

No comments:

Post a Comment