Monday, August 8, 2011

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akuta matatizo ya walimu wa sayansi chuo cha ualimu Matogoro Songea

 Makamu wa Mkuu wa chuo cha ualimu Songea Bi.Trefonia Nchimbi asoma taarifa ya chuo chake wa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo alipotembele chuo hicho kusuluhisha madai 7 ya wakufunzi wa chuo hicho.
Makamu huyo alisema chuo kina matatizo mengi yakiwemo ukosefu wa walimu wa sayansi Fizikia na Kemia Umeme katika masomo ya ITC,bwalo la chakula ni dogo lenye uwezo wa kuchukua wananchu 250 tu,Chuo hakina uzio kwa ajili ya usalama,na nyumba za watumishi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Philopo Mulugo akimsikiliza kwa makini Makamu huyo wa chuo cha ualimu anaposoma taarifa ya chuo hicho hapo juzi katika ofisi ya mkuu wa chuo hicho.

No comments:

Post a Comment