Sunday, August 7, 2011

MGOGORO WA WAKUFUNZI CHUO CHA UALIMU SONGEA UMEMALIZIKA NA WENGINE KULIPWA MWEZI HUU MWISHONI

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo,Jana alitumia busara katika kutatua mgogoro wa wakufunzi wa chuo cha ualimu songea kwa kufuatilia tatizo moja hadi kingine kwa kila mkufunzi,na hatimaye alibaini udhaifu uliyosababisha mgogogoro.
Alibaini uzembe wa utunzaji wa kumbukumbu wa walimu Wizarani,uongozi wa chuo kutokuwa makini katika kuelekeza wakufunzi ujazaji sahihi wa fomu za kupanda madaraja,Walimu wenyewe kutumia nyaraka za sasa kuomba madai ya sasa na hatimaye,ufinyu wa bajeti.Kwa wale ambao walihakikiwa watalipwa mwishoni mwa mwezi huu.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ualimu Bibi Hellena Lihawa  kiwaelekeza jinsi ya kukubali daraja na kuomba kulipwa baada ya kukubali daraja hilo.
 Afia elimu Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo mwenye miwani wakiteta jambo na Mkaguzi mkuu wa shule Nyanda za Juu kusini Bwana hadrian Mlelwa,baada ya baadhi ya wakufunzi kuvuka mipaka ya kinidhamu wakati wakielekezwa jinsi ya kutafuta suluhisho la mgogoro.
 Mkaguzi mkuu wa shule Nyanda za Juu Kusini Bw.hadrian Mlelwa akiwasini wakufunzi hao kuacha jaziba na kufuata kanuni za utumishi na kufuata maadili ya kazi ya ualimu.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu BibiFidelia Lukuna wizara ya elimu akisoma majina ya wakufunzi na walimu wa shule ya sekondari mazoezi na shule ya msingi mazoezi yaliyo kwisha hakikiwa na kubaini mapungufu kadhaa yaliyosababisha wasilipwe madai yao wakufunzi hao.







NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo amesuluhisha mgogoro uliyofanywa na wakufunzi wa chuo cha ualimu Songea wa kuacha kuingia madarasani kufundisha hadi walipwe madai yao wanayoidai serikali.

Mheshimiwa Mulugo amefuatilia mgogoro huo uliyoanza tarehe 27 Julai mwaka huu hadi leo sulihisho lilipo patikana baada ya kutafuta vyanzo vya mgogoro kwa kupitia kuuliza mwalimu mmoja mmoja na kugundua kuwa walimu hao baadhi yao wanadai kupanda madaraji na kucheleweshwa kulipwa mapunjo yao kwa wakati.
a kukaa katika daraja moja kwa muda mrefu,fedha za uhamisho na mizigo wakati wa kuhama,madai ya fedha za kusoma na makato yanayoendelea baada ya kuhama nyumba ya serikali.

Baada ya kupata maelezo kwa kila mdai ilionekana kulikuwa na mapungufu kadhaa yaliyo sababisha malipo yasifanyike kwenye madai yao.ambayo ni ufinyu wa bajeti,mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu wizarani si mzuri kwa kutokuwa makini katika kutunza kumbukumbu za mtumishi.

Mengine ni pamoja na kutokujaza nyaraka za madai kwa usahihi na umakini,kwa sababu walimu hawajui namna ya matumizi ya nyaraka za kuomba kulipwamadai yao.wengine walikuwa hawajui nini kifanyike baada ya kupewa daraja jipwa.

Mhe. Mulugo ametoa wito kwa watendaji wa idara ya utawala makao makuu ya wizara kubadilisha mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu za watumishi,kujibu mapema barua za watumishi,uongozi wa chuo uelekeze wafanya kazi wao jinsi ya kuomba masilahi yao.

Walimu waombe madai yao kwa nidhamu na busara hasa wanapo hitaji iwalipe madai yao,na TSD,REO waelekeze walimu jinsi ya ujazajiwa  fomu mbalimbali za madai kwa ufasaha.

Aidha Mhe.Mulugo amesema kuwa walimu nane ambao madai yao yamehakikiwa watalipwa fedha zao mwisho wa mwezi huu,malipo hayo yataendelea kulipwa kulingana na uhakiki uanavyoendelea wa kupitia faili moja hadi jingine.

Hatimaye Naibu waziri alitembelea chuo cha VETA Songea na chuo kikuu cha Sayansi ya Jamii .kinacho jengwa na maaskofu wa katoliki tawi na SAUTI kinacho tarajiwa kuanza Novemba mwaka huu,
 Na leo Naibu waziri huyo kaelekea Iringa wilaya ya Makete katika chuo cha ualimu Tandala.


No comments:

Post a Comment