RAIS Jakaya Kikwete amewataka
viongozi wa madhehebu ya dini nchini kishirikana na serikali katika kukemea
maovu yakiwemo ya biashara ya madawa ya kulevya ambayo yana haribu vijina ,pia
wanafunzi wa shule za msingu,sekondari amabo ndiyo nguvu kazi ya Taifa.
Rais
Kikwete alisema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Baraza la Eid
iliyofanyika kitaifa katika Msikiti wa Mkoa wa Dodoma leo akiwa mgeni
rasmi katika sherehe hizo za Eid,l alisisitiza kuwa ni wajibu wake
kukemea,kuonya na kutahadharisha hatari itakayo kuja mbele yake.
Alisema
kuwa tahadhari hiyo aliitoa siku ya kumweka wakfu askofu Jonh Ndimbo wa jimbo
la Mbinga kuwa baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na madawa ya kulevywa
na wengine walishikwa,wakiwemo watoto wa viongozi wa madhehebu ya dini.’Ilikuwa
ni wajibu wangu kukemea na tahadharisha wimbi la bishara ya madawa hayo kuingia
katika madhehebu ya dini’ alisisitiza Rais.
‘Viongozi
wa madhehebu ya dini zote tushirikiane katika mapambano haya ya kukemea maovu
yanayo sababishwa na biashara hii.’ Alisema Rais.Hili ni tatizo kubwa tunaomba
tushirikiane alisisitiza tena Rais.
Aidha
katika Baraza hilo
la Eid Rais alisema kuwa Serikali ina Mahakama yake hivyo haiwezi kuunda mahakama
nyingine,alipokuwa akiwaeleza Waislamu kuwa jambo la Mahakama ya kadhi bado linaendelea,anashughulikia Waziri mkuu
,wala hakuna mkono wa mtu.
Alisema
suala hilo litajadiliwa Bungeni,na Bungeni hakuna siri,kila mmoja atakuwa na
nafasi yake ya kuchangia suala hilo,wala siyo shinikizo la Baraza la Maskofu
ila wao walicho kisema nikuwa suala hilo liachiwe kwa waislamu wenyewe na siyo
serikali kuingilia musuala ya kidini.
Alisema
lengo la mahakama hiyo ni kwa ajili ya Talaka,Mirathi na wafu,si zaidi ya hayo
masuala yote yakijinai,madai,wizi yaachiwe kwenye mahakama ya serikali na siyo
mahama ya kadhi.
No comments:
Post a Comment