Monday, August 15, 2011

Utamaduni ,tudumishe ngoma zetu Lizombe au kitoto ukipenda toka kusini

 Jumatatu ya leo nawaletea utamaduni wa watu wa kusini,Wangoni hao na ngoma yao maarufu ijulikanayo kama Lizombe ama Kitoto.ni ngoma inayochezwa kwenye sherehe za kitaifa,kijamii.
 Hao ni waimbaji na wachezaji kwa wakati mmmoja,ni ngoma mabayo inayovutia kuiangalia,hasa katika miondoko yake,ona namna walivyo funga nguo zao kiunoni,ni kwa ajili ya miondoko,unajua kusimulia huwezi kufaidi,ili ukishuhudia mwenyewe miondoko yake,ndipo utakapo kubaliana nami,wajanja wanasema kunengua.
Hawa wanasanaa,sijui kwanini wasinge badilisha mfumo ukawa wa kisayansi zaidi,ili kuboresha kama wanavyo fanya wenzao wa makirikiri,kwakuwa makirikiri na Lizombe hilo hilo ila wenzao wamekuwa wajanja wanatengeneza fedha.

No comments:

Post a Comment