Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Injinia Monica Kebera akizungumza na waandishi wa habari wa Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ofisni kwake leo.kuhusu Rais Kikwete alivyo tekeleza ahadi yake kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma ya kutatua tatizo la umeme katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kuleta mashine mpya ya kuzalisha umeme.
Injinia Kebera akipata uhakika wa lini mashine hiyo itawasili Nchini katika bandari ya Dar es salaam kutoka Netherlands.kwa njia ya simu. ofisini kwake leo katika Manispaa ya Songea.
AHADI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kiwete ya kupeleka
mashine ya kufua umeme Manispaa ya Songea katika kituo cha kuzalisha umeme ( Power
Station )Kiblang’oma Lizaboni Manispaa ya Songea ameitekelea ya kuileta
mashine hiyo ambapo muda wowote kuanzia sasa itawasili bandari ya Dar es
salaam.
Akizungumza na Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ofisini kwake leo meneja wa TENESCO
Mkoani Ruvuma Injiania Monica Kebera alisema mashine hiyo ni mpya yenye uwezo
wa kuzalisha umeme wa KW 1,900
ambayo itawasili bandari ya Dar es
salaam tarehe 26 mwezi huu kutokea Neither land.
Injinia Kebera alisema mahitaji
ya umeme kwa watumiaji wa Manispaa ya Songea ni KW 4,500,ambapo mashine hiyo ikifungwa tatizo la umeme litapungua
kwa kiasi ingawa mgao utaendelea kuwepo kutokana na tatizo la taifa la
upatikanaji wa mafuta na mashine kufanyiwa matengenezo.
Alisema mataizo ya mgao wa umeme
ni wanchi nzima ila kwakipindi kilicho jitokeza cha kukosa umeme kabisa mjini
hapa ilikuwa ni kwa sababu ya ubovu wa mshine zake Kibulang’oma na upatikanaji wa mafuta kwa wakati.
Aidha Ijinjia Monica amemshukuru
Rais kwa ahadi yake aliyoitoa kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma ya kuleta mashine
mpya ya kuzalisha umeme ameitekeleza kwa wakatu mwafaka ,hata wakati tukisubiri
umeme wa grid ya Taifa lakini watumiaji wa umeme watakuwa wana matumaini
makubwa ya kupata umeme wa uhakika.
No comments:
Post a Comment