Thursday, August 11, 2011

Chuo cha Ualimu Songea cha kabiliwa na matatizo lukuki

 Baadhi ya wakufunzi na walimu kwenye masuluhisho ya mgogoro wao na serikali wakiwa na madai 7  wakimsikiliza naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo katika ukumbi wa chuo hicho.

 Makamu wa chuo Songea Bibi Triphonia Nchimbi akimkaribisha Naibu waziri wa elimu  Philipo Mulugo Songea chuo cha ualimu hivi karibuni.

CHUO  cha Ualimu Songea  pamoja na wakufunzi wake kuwa na mgogoro na Serikali lakini pia 
 chuo hicho kina kabiliwa na matatizo lukuki yanayofanya utendaji na ufanisi wa utoaji wa taaluma kuwa mgumu.

Makamu wa chuo hicho Bibi Triphonia Nchimbi alimweleza Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo alipofanya ziara ya usuluhishi wa mgogoro wa wakufunzi na walimu wa shule ya mazoezi za sekondari na msingi na serikali hivi karibuni.

Bibi Nchimbi aliyataja matatizo hayo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vitabu vya kisasa kwenye maktaba ya chuo yenye vitabu vingi vya zamani,umeme hasa katika kufundisha masomo ya ICT,mifumo ya maji safi na uchakavu wa  mfumo wa maji taka unaosababisha gharama kubwa katika kuyanyonya maji taka hayo.

Mengine ni pamoja na ukosefu wa kemikali za kutosha za kufanyia majaribio,vifaa vya maabara vya Fizikia,Biolojia na Kemia na vilivyopo vingi ni vya zamani na ukosefu wa mwangalizi wa maabara ( Lab Technician ).

Aidha alisema kuwa matatizo mengine ni pamoja na chuo kuwa katika hali hatarishi kwa kukosa Wigo (Fensi ),bwalo la chaula ni dogo na lazamani lililojengwa mwaka 1968 lenye uwezo wa kuchukua  wanachuo 270 tu.

Lingine ni ukosefu wa walimu wa sayansi hasa katika somo la Fizikia ambalo halina mwalimu hata mmoja na ukosefu wa nyumba za walimu ambapo kwa sasa kuna nyumba 21 kulinganisha na idadi kubwa ya walimu waliyopo.

Chuo cha ualimu Songea chenye wanachuo 516 wa Daraja la III A 309 na Stashahada 207 na wakufunzi 61 mkiwemo walimu wa kiume 46 na wakike 15.kilikumbwa na mgogoro wa wakufunzi na walimu wa sekondari mazoezi na shule ya msingi mazoezi kwa serikali kwa kuidai.

No comments:

Post a Comment