Sunday, August 7, 2011

MTAALA SI KITU CHA KUCHEZEA CHEZEA NI DHAMBI KUCHEZEA ELIMU– MTEGA

Mhshamu askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea akisalimiana na Mkaguzi mkuu wa shule wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw.Hadrian Mlelwa aliyekuwa kwenye msafara wa Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo alipo kwenye kutmbelea majengo ya Chuo kikuu cha sayansi ya Jamii jimboni humo jana jioni.


ASKOFU mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbeti Mtega anasikitishwa sana na kitendo cha wadau wa elimu nchini kuchezea chezea Mtaala wa elimu kwa kuubadilisha badilisha kila mara kitendo hicho kitaliangamiza taifa hili.

Mhashamu Norberti Mtega alisema hayo Jimboni hapo jana jioni alipomkaribisha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo baada ya chakula kilicho andaliwa kwa Naibu Waziri na baada ya kutembezwa kuona majengo ya chuo kikuu cha Sayansi ya Jamii katika Manispaa ya Songea.

Alisema kubadilisha mitaala kwa shule za msingi na sekondari kutawaathiri watoto hao kisaikolojia na kiakili,kwani nchi nyingi duniani zinaheshimu mitaala ya elimu  inayotolewa katika nchi yao.

Mtaala wa elimu haupaswi kubadilishwa kwa muda mfupi kwakuwa kubadilishwa kwa mtaala kunaenda sambamba na kubadilisha vitabu vya kiada na ziada jambo ambalo si jema kwa kuliandaa taifa kielimu,kikawada mtaala unatakiwa kukaa zaidi ya miaka 10 au 15 au zaidi.

Alisema mataifa mengine hutumia mwanya kama huo kulididimiza taifa,ili taifa ilo liangamie kwa kuwa na lisilo  watu wasio na elimu ya kutosho kwakuwa elimu ya msingi na sekondari si rika la kubadili mitaala,kwa vyuo vikuu hawa wana uwezo wa kuchambua ilipi baya na lipi zuri.

‘ Tutalijibia hili mbele ya Mungu kwa kuliangamiza taifa hili,kuchezea chezea mtaala wa elimu ni dhambi elimu si kitu cha kucheze,na sikitishwa sana kwa baadhi ya viongozi mara wapatapo dhamana katika Wizara ya elimu na kuanza kubadilisha mtaala wa elimu,hapa si mahala pa majaribio’.Alisema Mhashamu Mtega.






No comments:

Post a Comment