Saturday, August 13, 2011

TUSIDHARAU MICHEZO YA MAIGIZO/TAMTHILIA INASAIDIA KUENDELEZA UTAMADUNI WA MTANZANIA WABUNGE

Mbungea Mbeya Mjini Mheshimiwa Mbilinyi ( Sugu ) jana alisema fani ya muziki na sanaa nyingine zinalipa,Kinacho takiwa serikali kuwawezesha wana - muziki,wananii mbalimbali ili waliingizie taifa kipato.

Fani kama ya maigizo au sanaa za maonyesho ( Tamthilia ) zisidharaulike kwa kuwa zinasaidia kukuza na kuendeleza utamaduni wa - Mtanzania.


Michezo ya sanaa za maonyesho ( Tamthilia )  inakuza lugha ya Kiswahili, uzalendo wa jamii za wa – Tanzania kuendeleza utamaduni wanchi yetu

Wakati wabunge wakijadili bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni na Vijana masuala mengi yalijadiliwa yakiwemo matumizi ya lugha ya Kiswahili ,kuiga utamaduni wa wageni hasa katika mavazi,baadhi ya watu wanavaa mavazi ambayo yanaonyesha maungo ya ndani  au nusu uchi.

Na kazi ya sanaa na wasanii na jinsi sanaa inavyo weza kuwaondoa vijana kutoka kwenye vijiwe visivyo na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Naungana na wabunge kuwa vijana wakiwezeshwa katika sanaa ya muziki,uchoraji,ususi,na michezo ya kuigiza mipira kandanda ,wanaweza kapata fedha kwakuajiriwa au kujiajiri au  kuuza kazi zao,na kazi zao zisiibwe na watu wengine ikiwa sheria zitafuatwa za kuheshimu kazi ya msanii.

Wageni wlivyoingia nchini walikuta wa- Tanzania  wakiwa na sanaa za maonyesho ambayo ilikuwa urithi wa utamaduni wa Kiswahili ,hasa katika kufundisha wasichana kwa njia ya unyago, jinsi atakavyo weza kuishi na mme wake kama mtu mzima.

Shangazi na akina mama ndiyo walifundisha hao wasichana kwenye chumba cha siri ambapo wanaume hawakuruhusiwa kuingia..Aidha kulikuwa na michezo ya kienyeji hasa katika shughuli za kijamii.

Shughuli hizo ni pamoja na arusi,mazishi,mavuno,ujenzi na kilimo.Lakini zilikuwa ni Fasihi simulizi,walipoingia wakoloni wazungu walileta fasihi andishi.wakatumia michezo hiyo kwa kujistarehesha.Na kuwadharau waafrika,ambapo waliwatunia waandishi wa fasihi andishi kukashifu uafrikana uafrika wao na wao walikuwa wazungu weusi.

Fani hii ya michezo ya kuigiza imesaidia kuendeleza na kusambaza utamaduni wetu,ingawa wazungu walipofika waliathiri maudhui ya fani ya sanaa ya maonyesho na jukwaa lake.


No comments:

Post a Comment