Friday, February 25, 2011

TAMASHA LA KUMBUKIZI YA MASHUAA WA VITA VYA MAJIMAJI NA UTALII WA UTAMADUNI LIMEANZA LEO MJINI SONGEE

 Tamasha hilo limeanza na wageni mbalimbali kutoka Tanzania na Msumbiji,wanaoingia ukumbi wa Songea Club Ni Mhe.Dr Christine Ishengoma Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katikati, mwenye kiti wa Bodi ta makumbusho ya taifa Dr.Constancia Rugumanu Kulia na katibu Mkuu wa Wizara mali asili na utalii  kushoto.

Kaimu RAS mkoa wa Ruvuma Dr.Tarimo akimkaribisha Mwenyekiti wa bodi ya makumbusho ya taifa Dr.Rugumanu,kutambulisha wageni,aliwatambulisha wageni wengi akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Ujumbe kutoka Msumbiji na wageni wengine.
 Mwenyekiti wa Bodi ya makumbusho ya Taifa Dr.Onstancia Rugumanu akitabulisha wageni katika ukumbi wa songea club leo.
 Katibu mkuu wizara ya maliasili na Utalii akisalimia wajumbe na wanakamati wa sherehe.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Lichinga Nchini Msumbiji Mhe.Augusto Assifue na ujumbe wake wa watu watatu waliyo wakilisha nchi ya msumbiji.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora bwana Abedi Mnyemusa akisalimia wajumbe wa maandalizi ya Tamasha.
 Mkuu wa wilaya ya Nkansi Mkua wa Rukwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Bw.Daniel Ole Njolai
Chifu wa kingoni Bambo Emmanuel Zulu Gama akiwasalimia wageni na wajumbe wa Tamasha hilo,ambalo limeanza na ziazra ya kutembelea vivutio vya utalii vya :-
  • Chandamali.
  • Luhira
  • Peramiho
  • Maposeni,baada ya kukabidhi gari kituo cha Makumbusho ya majimaji cha Songea.kilele ni siku ya tarehe 27/2/2011.katika mnara walionyongwa machifu wa kingoni.Ambapo kutawekwa silaha za kijadi,mashada ya maua.na kuonyesha kazi za mikono.

Thursday, February 24, 2011

MWANAFUNZI WA MIAKA 12 KUWA MKE WA TATU WA MZEE VISENTI HAULE

Binti wa miaka 12 katikati Veronika Charlle wa darasa la tano, akiwa na mwenye kiti wa kijiji cha Sinai Talisis Mkanula na mhudumu wa afya  msingi Christina Njovu.walijaribu kumsaidia mtoto huyo lakini kukawa na urasimu wa kushindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa Bwana Vinsenti Haule kwa kesi ya ubakaji maana huyu mtoto ni sawa na mjukuu wake.


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Vinsenti Haule mkazi wa kijiji cha Sinai Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma ambaye ana wake wawili amemuoa mwanafunzi  wa darasa la tano wa shule ya msingi Nakahuga  Veronika Challe(12) kuwa mke wake wa tatu.Imeripotiwa  na Albanos Midelo.

WALIPONYONGWA NDUNA WA WANGONI NA WAKOLONI PAMEJENGWA MNARA WA MAKUMBUSHO



 ,Mnara huo kwa mbele ,hapa ni karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma eneo la kihistoria ambapo viongozi wa kabila la kingoni waliponyongwa na wakoloni.
 Hapa nyuma ya mnara ambapo kuna nguzo na mwamba wenye kamba walizo tumia kunyonga viongozi wa kingoni.
 Mazingira ya mnara huo kama unavyo onekana kwa karibu.
Mzee Joseoh Henjewele mwenye fimbo ambaye pia alikuwa diwani mwanzilishi wa Mji wa Songea mwaka 1974,anasema tunaishukuru serikali kujenga kumbukumbu eneo ambalo babu zetu walinyongwa, lakini katoa anaglizo kuwa mnara ulivyo pakwa rangi ya kijani hakuleti uhasilia wa jambo lenyewe kihistoria ya wangoni.

Mahali damu ilimwagika ilitakiwa ipakwe rangi nyekudu ili kuondoa dhana ya mnara huo vinginevyo inaonyesha ni wa kumbukumbu ya kuzaliwa,kwa,CCM  kwani rangi zilizopakwa zimepoteza maana kabisa kwa tukio la kunjingwa kwa wangoni mahali hapo.

Wednesday, February 23, 2011

ZAIDI YA WANAFUNZO 5,000 WILAYANI KILWA WALIOMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA JANA HAWAJUI KUSOMA

Kufuatia kikao cha tathimini ya elimu wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi kimebaini kuwa wanafunzi zaidi ya 5,000 wilayani humo waliomaliza elimu ya msingi mwaka 2010 hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu,jambo ambalo liniongeza idadi ya watu wazima kuto jua kusoma.

Uongozi wa elilmu wa wilaya hiyo umebaini kuwa tatizo lililo fanya matokeo hayo ni wazazi kutokuwa na mwamko wa elimu,watoto wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo,uvuvi na uchungaji,ambao ni utoro uliokithiri.

HOMSO/ HOSPITALI YA MKOA SONGEA KIPINDI KIFUPI CHA MGANGA MKUU DANIEL MALEKELA

 Daktari Daniel Malekela akitoka jengo jipya la wazazi ambalo lina chumba cha upasuaji wa mama mjamzito aliyeshidwa kujifungua mwenyewe.Daktari Malekela anasema kwa siku watoto 30 huzaliwa katika Hospitali ya mkoa  Songea.
 Kwa muda mfupi tu wa uongozi wa mganga mkuu huyu wa mkoa Daktari malekela kwa uongozi wake na staff yake na uongozi wa mkoa ameweza kubadilisha mazingira ya Taasisihiyo ya Afya ya mkoa wa Ruvuma kwa kufanya ukarabati mkubwa na kujenga majengo mengine mapya likiwemo hilo la ghorofa na jengo la wazazi. 

 
Majengo yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa ni pamoja na jengo la upasuaji la zamani pamoja na OPD na majengo mengine ambayo Mganga mkuu huyo alimtembeza mpiga picha wa Blog hii kujionea maajabu.

BREAKING NEWS UMOJA WA WAZEE TUNDURU WAIOMBA SERIKALI MIKOPO YA KUNUNULIA MATREKTA MADOGO ( POWER TILLER )


UMOJA wa Wazee na Wastaafu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma (CHAWATU) waomba serikali iwapatie mikopo ili kuwa kwamua katika lindi la uaskini.

Wazee hao walimweleza Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Juma  Madaha kuwa wakipewa mikompo hiyo wanunua matrekta madogo (Power Tiller),kulima shamba la alizeti lenye ukubwa wa Hekta 50 pamoja na pembejeo za kilimo

MUZIKI MZURI NI MUHIMU KUWA NA ALA ZA MUZIKI ONA KWAYA YETU

 Pamoja na kuwa na kinanda pia waumini wa kigango cha matarawe kimeweza kujichangisha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa lao,na hatimaye sasa wanaendelea kwa ajili ya kupiga lipu.
 Hicho ni kikundi cha kwaya hiyo,wamevaa sare tofauti kidogo na zile za pinki ndiyo manjonjo hayo katika kufanya kwaya iwe ya kuvutia machoni kwa watu.Muziki sio uhuni alisema Hayati Remi Ongala.Maana unaliwaza,katika maombolezo,katika kumuomba mungu.na katika starehe mbalimbali.
Kwaya  ya Kigango cha Matarawe kimemudu kununua kinanda chake ili kiweze kukoleza harmony ya mziki wao.Ni nguvu za waumini wenyewe katika kufanya ibada iwe na uhai.

NI MAMBO YA WATOTO HAYO,KUANGUKA KWA MTI NI FURAHA YAO

Camera yetu iliwakuta wanafunzi  hawa wa shule ya msingi Matarawe Manisoaa ya Songea Mkoani Ruvuma hivi karibuni , wakipanda juu ya matawi ya mti mkubwa uliyokuwepo shuleni kwao,ambao uliangushwa na upepo usiku wa siku hiyo.Hivyo kipindi cha mapumziko cha wanafunzi hao walipata nafasi ya mchizo wa kupanda kwenye matawi hayo na kutambiana ninani anaweza akawa bingwa wa kupanda kwenye miti?.Hayo ndiyo mambo ya  uanafunzi na Utoto wa utafiti wa kutaka kujua mambo hata ya hatari kwao.

Tuesday, February 22, 2011

BREAKINGNEWS WAHADZABE KUJENGEWA HOSPITALI IRAMBA SINGIDA

Shirika la Wamarekani limetoa mchango wa  shilingi milioni 25 kwa ajili ya kujenga hospitali kwa ajili ya kuwasaidia  kabila la Wahadzabe wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida hivi karibuni.

MAFUNZO YA COMPUTER NA ADA YAKE NI POA FIKA UTONE OK . SONGEA MJINI

 Kutana na wanafunzi wanafunzi ambao wako darasani kwa mafunzo ya vitendo,mafunzo hayo yapo katika hatua kadhaa ambayo yameainishwa katika jedwali  hapo chini na gharama zake kwa kila Program.
 Sayansi na teknolojia ya sasa ni muhimu kujua matumizi ya Computer hatau kwa hatua,Utanadawazi maana yake ni kujua matumizi ya Computer,haijalishi umri wa mtu,wala elimu ya mtu,kwa bahati nzuri au mbaya msomi wa elimu ya kuu kabisa lakini matumizi ya computer yakampitia kisogoni sasa wakati ni huu.
Vijana nao hawapo mbali kwa kujifunza Computer,hawa ni baadhi ya wanafunzi wa chuo hiki mashuhuri sana hapa Manispaa ya Songea.Isitoshe Mkurugenzi wa Chuo hiki ni mtaalamu wa Instolation of Computer and Ant Vuirus kwnye computer Mr.Mpele Soka.

EASY  TECH.COMPUTER TRAINING CENTRE

Chuo cha Easy Tech.Computer Training Centre ambacho kipo ndani ya manispaa ya songea  kinatoa mafunzo ya computer kwa kozi  zifuatazo:

No:
kozi
muda
Ada
1.
CERTIFICATE IN OFFICE APPLICATIONS
15 WEEKS
180,000/=
2.
CERTIFICATE  IN COMPUTER REPAIR  AND MAINTENANCE
2MONTHS
200,000/=
3.
CERTIFICATE IN ACCOUNTING PACKAGE-  (PASTEL,TALLY OR M.Y.O.B. AND QUICK BOOK).
@ 3 WEEKS
80,000/=

 Ndani ya  hiyo kozi namba 1  kuna program zifuatazo
ü      Introduction to computer kwa Tshs.  20,000/-

ü      Ms. word  kwa  T.shs 25,000/=

ü      Ms Excel   kwa Tshs.25,000/=

ü      .Ms PowerPoint kwa  T.shs 25,000/=

ü       Ms. Access  kwa T.shs. 25,000/=

ü      .MS.Publisher  kwa T.shs. 30,000/=

ü      .Internet and Email  kwa 30,000/-                                   
Pia tunatoa fomu  ya kujiunga na chuo kwa shilingi 2000/= tu

Chuo kinawakufunzi waliobobea kwenye fani ya computer, kinatoa ofa  kwa atakaye weza kulipia programme 6 kati 7 za computer kwa mara moja atapata kusoma programme ya  kwanza bure ( introduction to computer)  wahi sasa nafasi ni chache  bei zetu ninafuu sana.



Malengo  yetu  ni kuhakikisha mtu anaelewa wala siyo kumaliza programme chuo kimenuia  kwa dhati kabisa kutoa  elimu bora ili kuendana na ulimwengu wa sasa wa teknologia ya mawasiliano ya computer.  (IT)



Chuo kinapatikana katika jengo la ok hotel  mkabala na  wa Krister Park (fast Food )  songea mjini. Karibu na kanisa la Lutherani (KKKT usharika wa kanda ya kusini)

watu wa rika zote mnakaribishwa njooni mjionee tofauti kwa kupata elimu bora inayokidhi matakwa yako kwa bei nafuu sana. na muda mfupi.

Kwa Mawasiliono Zaidi Piga Simu : 025 2602428, AU SIMU YA KIGANJANI:(0713/0752/0787) - 440996


N.B :_-Nimetuma  picha tofauti ili  uchague zipi zinafaa

KIPINDI CHA MVUA KILIPOCHELEWA WAKAZI WA SONGEA WALIKWENDA KUOMBA MVUA KWA AKINA NKOSI NA NDUNA WAWA NGONI MATOKEO YA MVUA HIZO NI HAYO:

 Mvua zilipo chelewa wazee wa kingoni walikwenda kuomba mahoka kwenye makaburi ya machifu wa kingoni kwa jina maarufu Nkosi,Nduna kwenye Makumbusho ya Taifa ya Majimaji,na matokeo yake mvua zilinyesha,lakini ziliambatana na upepo mkali,nyumba zilibomoka,uribifu mkubwa pia ulifanyika.
Moja ya jengo la shule ya sekondari Muslimu hapa Songea,nusura liangukiwe na na mti huo kama unavyo uone.

VIJANA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA SONGEA

Asiyefanya kazi na asile Imeandikwa kwenye vitabu vitakatifu,ili kutimiza usemi huo haijalishi mtu anafanya kazi gani,kamira yetu iliwakuta vijana hawa wako kazini wakipeleka mifuko ya mbolea ya kukuzia mahindi kwenye shamba la mteja wao.Katika Manispaa ya Songea hapo jana,

Vijana hao walipita jirani kabisa na nguzo ya simu ambayo ilipata msukosuko wa upepo mkali uliyoandamana na mvua.hapo  jana.

Matukio ya hapa na pale katika anga za elimu nchini

Mbunge wa zamani Kalenga George,ameiambia serikali kuwa kama inataka maendeleo mazuri ya shule za sekondari  ni lazima ifanye kiwsahili lugha ya kufundishia,

Monday, February 21, 2011

UTANDAWAZI NA MATUMIZI YA BLOG FACE BOOK KWA VIJANA WA LEO

Mhariri uzalishaji wa Magazeti ya HabariLeo Bwana Beda Msimbe ( likwangule entertainment ) mtumiaji mkubwa wa blog na amewafundisha wengi matumizi ya blog na face book.


Ulimwengu   wa vijina wa leo niwablog,vijana wengi hivi sasa wanatumia Blog, Face book, na mitanadao mingine kupeleka ujumbe na kufanya mawasiliano pembe zote za dunia.kupitia mtandao wa Internet.

Mhariri uzalishaji wa magazeti ya HabariLeo Bwana Beda Msimbe alisema  hayo siku ya mdahalo wa waandishi wa habari na wadau wa habari Mkoani Ruvuma hivi karibuni.Alisema wazazi kuwa na kompyuta ( computer au laptop ) kutamsaidia sana mtoto kuielewa na kuitumia vyema.Maana matumizi ya blog na Face book  yameongezeka na yana zidi kuongezeka kila kukicha.katika ulimwengu huu wa utanda wazi.

PERAMIHO TRADE SCHOOL NI UKOMBOZI WA VIJANA

Trade school Peramiho ni ukombozi wa vijana wanaopitia katika chuo hicho kuhitimu mafunzo yao ya ushonaji wa nguo za akila aina,hasa wamebobea katika ushonaji wa suti.Wanakwenda kujiajiri wenyewe na wana soko sana hasa katka ushonaji wa suti.

Chuo hiki kipo Permiho kinatoa mafunzo katika fani za Ushonaji wa nguo, seremala,uashi,bomba na makenika.Sasa kinafundisha na masomo ya ziada ya hisabati,kiingereza na kiswahili na wanafanya mitihani ya VETA.

TRANSFORMA LA UMEME NUSURA KUANGUKA MAENEO YA MATARAWE MANISPAA YA SONGEA JANA

Transforma hilo lilipata dhoruba ya upepo mkali,afisa mmoja wa shirika hilo anawasiliana na wenzake kufika katika tukio kulisimamisha, maana mvua za upepo sasa zinatishia amani katika manispaa hii.

DIWANI APONGEDWA KWA USHINDI WAKE

Mwandishi wa habari mkongwe Bwana Thomas Lipuka kushoto na mwenye kiti wa Ruvuma Press Club Bwana Juma Nyimayo kulia wanampongea Diwani wa viti maalumu CCM  Kata ya Mahanje Madaba Songea Vijijini Mhe.Atonia Mselewa,kwa ushindi aliyoupata.

Aidha walimsifu aliposema kuhusu  masuala ya marumbano na madiwanai wa vyama vya upinzani ndini ya vikao hauna tija kwa kuwa wote wametumwa kuwa wawakilishi wa wananchi katika vikao hivyo,na siyo marumbano.

MVUA YA UPEPO YALETA MADHARA OFISI YA TUJIFUNZE SONGEA MJINI JANA

 Hayo ndiyo madhara ya mvua ya upepo katika Manispaa ya Songea jana,nyumba nyingi zimeezuliwa,nyingine zimeanguka,madish ya TV yamerushwa mbali,nguzo za simu na umeme zimeangushwa
Wafanya kazi wa ofisi ya TUJIFUNZE wameikata miti iliyo  angukia paa la ofisi na uliyoangukia choo cha TUJIFUNZE Kusini baada ya kuangushwa na upepo mkali uliyoandamana na mvua katika Manispaa ya Songea jana.

Sunday, February 20, 2011

HABARI NJEMA JUMAPILI YA LEO KWA WANADAMU,TUSIWE WATU WA KULIPA VISASI KWA WENZETU

 Katika kuazimisha misa katika kigango cha Matarawe Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma Padre Nicodemus Mbano,alisema katika mahubiri yake kuwa binadamu tusiwe watu wa kulipiziana visasi,kwa Mungu anafanyiwa makosa mengi na wanadamu lakini halipizi visasi ila anawapenda na kuwaongezea zaidi wakiomba.

Amesema visasi vikishamiri ndoa zinakuwa mashakani,isitoshe sikuhizi wanandoa kuachana imekuwa fashion,Aidha amewasifu waumini wa kigango cha Matarawe kwa jitihada zao.kikiwemo na kitabu cha kuendeshea ibada za misa ambacho amekishika.

 Padre Nicodemus Mbano  akimkabidhi mwenye mweka hazina wa kigango card ya kushiriki Jubilei ya miaka 25 ya Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea tarehe 9/6/2011.
Padre Mbano pia ni Padre wa miito mitakatifu jimboni.Bwana ni mwenye huruma,hivyo nasi tuwe na huruma kwa wenzetu..

TUNAKUOMBEA HERI ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA SONGEA NORBERT WENDELIN MTEGA JUBILEI YA MIAKA 25 YA UCHUNGAJI

Jimbo kuu la Songea Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhasamu Norbert Wendelin Mtega atadhisha Jubilei ya miaka 25 ya Uchungaji katika nafasi hiyo toka mwaka 1986  hadi mwaka 2011.

Waumini wote wa Jimbo Kuu la Songea na wengine popote pale walipo, tarehe 9/6/2011 watakuwa na adhimisho la kumshukuru Mungu:Jubilei ya miaka 25 ya utumishi wa Askofu Mkuu Norbert Mtega.Ili kufanikisha shughuli hiyo  kubwa muhimu ya kiimani  ya Uchungaji  kwa yeyote atakaye guswa na tukio hilo atapeleka mchango wake namba ya simu.0712 920955.kwa  Pd.Camillus Haule Naibu wa Askofu Mkuu.Kutoa ni moyo nawala siyo utajiri.

Ee nafsi yangu  umuhimidi bwana…wala usisahau fadhili zake. Zab.103: 1-2

Saturday, February 19, 2011

NAULI MPYA ZA MABASI JIJINI MWANZA ZINAWEZA KUANZA KUTUMIKA KUANZIA KESHO

Baada ya madereva  Jijini Mwanza kugoma tarehe 16 mwezi huu,SUMATRA yapandisha nauli za mabasi ambazo zitaanza rasmi kuanza kazi kuanzia Jumatatu ya kesho.

BREAKINGNEWS !! RAIS YOWER MUSEVENI WA UGANDA AONGOZA KWA ASILIMIA 70

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anaripotiwa kusinda kwa asilimi 70 kuanzia sasa dhidi ya mpinzani wake Kizza Besigye katika uchaguzi unaoendelea nchini humo.

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI IMEMTEUA BWANA FRIDOLIN BANZI KUWA MKUU WA KITUO CHA PRESS A MAGOGONI DAR ES SALAAM


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imefanya Uteuzi wa Bw. Fridolin Banzi kuwa Mkuu wa Kituo cha Uchapaji Dar es Salaa, ‘Press A’
Kabla ya Uteuzi huo, Bw Banzi (Pichani) alikuwa Mkuu wa Kituo cha Nyanda za Juu Kusini- Mbeya, ambacho kinatoa huduma kwa mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa.

Kituo cha Uchapaji Dar es Salaam ‘Press A’ ndicho Kituo kikuu cha vituo vyote vya uchapaji hapa nchini vinavyomilikiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kilikuwa kikiongozwa na Bw Mwalimu Saleh, ambaye alistaafu Utumishi wa Umma mwaka uliopi


Mhariri: Tunakutakia mafanikio katika nafasi yako mpya.

DEREVA HANA UJANJA KWA TRAFIC BARABARANI

Maadili ya kazi yanatoautiana kwa kila sekta,maadili ya dereve yafanani na maadili ya karani,au maadili ya Trafic barabarani hayafanani na maadili ya mwandishi wa habari,ingawa wote wanaajira.Kwa hiyo hakuna haja ya kuponda maadili ya kazi ya mtu mwingine.cha msingi ni kufanya kazi yako kwa kuheshimu maadili na miiko ya kazi yako.

Trafic lazima akusimamishe kuhakikisha unafuata sheria na kanuni za usalama barabarani? umekamilika katika kukiendesha chombo cha moto?.kama sivyo atakutia hatiani ,kwakuwa katimiza wajibu wake,asilaumiwe.Barabara na usalama wa raia ni jambo la msingi kwa waendesha vyombo vya moto.

Friday, February 18, 2011

BREAKINGNEWS VIONGOZI WA DINI JIJINI DAR ES SALAAM WAIOMBEA TANZANIA AMANI

 Viongozi hao wa madhehebu mbalimbali walikuwa na mktano wa kujadili na kuweka mikakati ya kuwepo kwa amani nchini,baada ya na kable ya kikao hicho kulifuatia na maombi na duwa kutoka kwa viongozi hao.
 Mwaenye kiti wa mkutano huo Shekhe wa Msikiti wa  Jijini Dar es salaam kabla ya kufunga mkutano huo aliwasome wajumbe wa mkutano huo maazimio 10 yatokanayo na mkutano huo.Alisema viongozi wa dini tusiwe chanzo cha uvunjifu wa amani miongoni mwetu.Mitume wote walikuja duniani uleta amani kati binadamu.Aidha alisema mkutano huo ulikuwa wa viongozi wa dini wa Dar es salaam peke yao.
 Mgeni rasmi mwenye kiti wa makampuni ya IPP Bwana Regnal Mengi alisema Tanzania ni kisiwa cha amani hivyo ni juu ya viongozi wa dini kuhubiri amani,ili taifa liwe na amani.'alisema nchi ikiwa haina amani wenye kutengeneza silaha wanafurahi kwa kuwa watapata soko la kuuzia silaha zao ili mmalizane'alisema Mengi.
 Mashekhe,maaskofu,wachungaji wa jijini Dar es salaamu walichangia hoja hiyo.walisema serikali na viongozi wa dini wako mbalimbali,ndiyo maana kunapotokea jambo muumini akimuuliza kiongozi wake hajui,hivyo ni muhimu serikali iwe karibu na viongozi hao.
Baadhi ya viongozi wa dini wakisikliza kwa makini mazungumzo.

kutana na Machifu wa Kingoni Nduna

Viongozi wa Kingoni wakiwa na  watawala wa Kijerumani,Nduna Mbano Songea hakupenda utawala wa kijerumani kwa kuwa  na utawala wa kimabavu.kwa kukataa  utawala huo.Machifu 66 waliuawa na kuzikwa katika kaburi moja.Isipokuwa Nduna Mbano Songea alizikwa katika kaburi la peke yake.

KUPATA MAVUNO MENGI LAZIMA KUTUNZA SHAMBA LEO NAMKUTA MKULIMA WA MAHINDI SONGEA

Kwa mujibu wa wataalamu wa kilimo Mkoani hapa wanashauri mkulima kupalilia shamba lake kuondoa magugu,kuweka mbolea ya kukuzia ili kupata mavuno mengi na ya uhakika.

Mkoa huu unachukula cha kutosha ghala yataifa la kuhifadhi chakula Ruhuwiko kuna mahindi mengi ambayo sasa yanapelekwa Dar es salaam.Ila wafanya biashara wenye malori makubwa wa Mjini Songea hawakupata tenda ya kupeleka mahindi hayo Dar es salaam.isipokuwa watu wa Dar es salaam.Je wakati wa kuyasomba mahindi kipindi cha mavuno mwaka huu watakuja wao kuyasomba?.

Je hiyo tenda imetolewa kwa njia zipi? wasafirishaji mjini hapa wanakilio kikubwa kwa kutotendewa haki kama wafanya biashara wa Mkoa huu,hawapati jibu .

MAKAO MAKUU YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA UPANGA KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI LEO

Mkuu wa wa usalama na utambuzi  Brigedia Jenerali Paul Meela ametota taarifa ya kwanaza kufuatia milipuko ya mabomu  Gongo la Mboto juzi,  kwawaandishi wa habari makao makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania Upanga  kuwa Ghala namba 5 ndiyo lilianza kulipuka,saa 2.30 usiku ndipo maghala yote 23 yalilipuka hadi saa 10.30 alfajiri na kuleta maafa  ya watu 20 na majeruhi 335.

 Alisema Taifa limepata hasara kwa wananchi walioyo poteza maisha yao na majeruhi waliyo athirika katika tukio hilo.Alisema ni mapeme mno kujua chanzo chake ila wananchi wawe na subira kupata chanzo cha milipuko hiyo.
Alisema mabomu yanaweza kulipuka kwa sababu mbalimbali kama hali ya hewa,uzembe au kulipuka yenyewe.
 Waandishi wa habari walitaka kujua kuwa matatizo kama hayo yanajirudiarudia ,kuna nini,kama ndivyo wanachukuliwa hatua gani waliokuwa wakilinda siku hiyo ?
 Brigadia Jenerali Leonard Mndeme,aliwaambia wandishi wa habari kuwa si kweli mabomu yalihifadhiwa kama mahindi,bali mabomu hayo yamehifadhiwa kitaalamu na wanayo yatunza ni wa taalamu wa milipuko.

Aidha alisema kuwa matukio kama hayo yametokea Zambia,Mozambiki,ni jambo la kawaida mabomu kulipuka,bila kutambua kuwa sasa yanalipuka.
Waandishi wakadadisi kuwa isiwe ni hujuma tu ilifanyika kati ya wapiganaji kwa kuto kuchukua taadhari ya milipuko hiyo,au siasa imeingia majeshini.

Idha Brigedia Jenerali Paulo Meela alisema watu 4,000,000 walifika uwanja wa uhuru kutamba ndugu  zao,majeruhi walipelekwa katika hosipitali za Temeke,Amana na Mhimbili. Amewataka wananchi kuacha kuokota kitu wasicho kifahamu.