Dunia ni matokeo ya uumbaji wa Mungu,ambayo viumbe vyote vimo ndani yake,vyenye uhai na visivyo na uhai.Lakini kuna Tafsiri nyingi zilizotolewa na Maandiko mbalimbali ya vitabu vya Dini,na wanasayansi katika kuielazea Dunia.
DUNIA ni moja wapo ya sayari
ambayo iliyokamatia uhai wa viumbe vyenye uhai na vitu visivyo na uhai.Na kubwa
zaidi kuna binadamu ambaye aliambiwa na Mungu avitawale vitu vyote vilivyomo
katika Dunia,kwa kuwa kapewa akili na utashi.
Kwenye ardhi viumbe hai ni
vingi ambavyo tunaamini wanasanyansi wameshavibaisha kwa mamilioni yake,
wanyama kwa makundi yake,ndege warukao na wale wasio na uwezo wa kuruka
kutokana na uzito wao kama mbuni,kuna mimea,kuna miamba,kuna maji ambayo
yameitwa bahari,mito,mabwawa,chemichemi.
Sifa za dunia kuwa na majira
mbalimbali katika mwaka,kutokana na kuinama kwake kwa digrii 23.5.Hilo hufanya
kuwe na viwango mbalimbali vya hali ya hewa joto au baridi.Mwinamo wake katika
mhimili wake umeonekana kuwa bora kabisa,ili kuendeleza uhai.
Je ni kweli Dunia inamzingo
wakilometa 40,000 na inazunguka mara moja kila saa 24.?
Je maeneo maeneo yaliyo
kwenye Ikweta au karibu yanasonga kwa kilometa 1,600 hivi kwa saa?
Ni kweli Dunia inazunguka jua
kwa kilometa 30 hivi kwa sekunde? Ambapo mfumo wa jua kwa ujumla unazunguka
kitovu cha kilimia kwa mwendo wenye kustaajabisha kwa kilometa 249 kwa
sekunde.Je unaweza kulinganisha na risasi inayosafiri kwa mwendo unaopungua
kilomita mbili kwa sekunde?
Hayo mambo ya Sayari ambazo
ni kazi ya Mungu,aliye umba mbigu na Dunia na ndani ya Dunia hiyo kaumba vumbe
vyenye uhai na visivyo na uhai.Ambapo kamuumba Binadamu atawale vitu hivyo vya nchi kavu na vya
majini.Baadhi ya Binadamu hao ndio wanasayansi ,walijaribu kubuni vitu
mbalimbali na wakaweza ila wakashindwa kumtengeneza binadamu mwenzao ambaye
angefanana na wao,Unadhani kuna siku huyu binadamu anaweza kuumba binadamu
mwenziwe?.
No comments:
Post a Comment