Thursday, March 17, 2011

HEKAHEKA ZA KUBORESHA ELIMU WILAYA YA MBINGA MKOA WA RUVUMA ZIMEPAMBA MOTO

Wanafunzi wa shule ya msingi walemavu Huruma Mbinga mjini wakiimba wimbo wa shule kwa wageni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walipo tembelea shuleni hapo mwaka jana.



Wilaya ya Mbinga  Mkoani Ruvuma yenye Tarafa 9 na kata 49 zilizotokana na kuongezeka kwa Tarafa tatu na kata 12 baada ya kuzaliwa Wilaya mpya ya Nyasa,ina shule za msingi 318 zenye wanafunzi 100,925 kati yao wavulana 50,498 na wasichana 50,527 ni wilaya yenye maendeleo mazuri kitaaluma na changamoto zake katika uboreshaji wa taaluma mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Tathmini ya elimu ya Mbinga na Mpango wa mwaka 2011 juu ya uboreshaji wa Taaluma inaonyesha kuwa wilaya ina upungufu wa walimu 424 sawa na uwiano wa 1: 40.kati ya walimu 2,159 waliopo.

Aidha mwaka 2010 wilaya ilipewa mgao wa walimu 22 ambao wote wamepangiwa shule zenya upungufu,sambamba na hilo watoto 12,259 wakiwemo wavulana 6,131 na wasichana 6,128 wameandikishwa  kuanza darasa la kwanza mwaka huu,kati ya watoto 16,216 kati yao wavulana 8,236 na wasichana 7,980 waliotarajiwa kuandikishwa shule.

No comments:

Post a Comment