Tuesday, March 1, 2011

HABARI KWA UFUPI WATOTO 300 WAKAA CHINI KWA KUKOSA MADAWATI TUNDURU

Wazazi wakikosa mwamko wa elimu katika jamii mambo mengi yatakwama katika maendeleo ya elimu ya watoto nchini,Wazazi wa shule ya msingi na ufundi Mataka hawa taki kuhudhuria vikao,kutoa michango ya kununulia madawati.hawa ni baadhi ya wanafunzi 300 walokosa madawati shuleni hapo.

   SHULE ya msingi na ufundi Mataka iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma inakabiliwa na upungufu wa madawati 100 hali iliyosababisha wanafunzi 300 kukaa chini.
    Mwalimu mkuu wa shule hiyo Hassan Nakoma alisema hivi karibuni kuwa shule hiyo ina wanafunzi 768 kati yao wasichana 350 na wavulana 418 na kwamba idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la tatu na nne wanakaa chini.
    “Hali ni mbaya zaidi katika darasa la tatu ambalo lina madawati manne tu ambayo yanawezesha kukaa watoto wanne kila dawati hivyo  watoto wengi wanakaa chini,tumezungumza na wazazi  na kuwaita katika vikao hawafiki na wameshindwa kuchangia hadi sasa wazazi watatu tu ndiyo wametoa fedha sh,15,000 sawa na kununua madawati matatu tu,kamati ya shule ipo lakini  wazazi hawana mwamko katika elimu”,alisema.( source Albano Midelo Tunduru )
 

1 comment:

  1. Tunduru ina umaarufu duniani kwa madini ya thamani. Nchi imekosa sera na uongozi bora. Wakati watoto hao wa Tunduru wanateseka hivi, watu wa nchi za nje wanachota madini Tunduru na kutajirika kwenye masoko ya kimataifa. Mfano ni huu hapa.

    ReplyDelete