Wilaya ya Mbinga imeweka
mikakati ya kuinua kiwango cha taaluma ya elimu ya sekondari ambapo wilaya ina shule za sekondari 60 kati yake shule 51
zinamilikiwa na serikali na Halmashauri, na 9 zinamilikiwa na mashirika ya dini
na watu binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa ya kutathmini elimu ya wilaya hiyo inaonyesha
kuwa wilaya ina wanafunzi 23,140 kati yao wavulana 12,003 na wasichana
11,137.katika idadi hiyo wanafunzi walemavu wa aina mbalimbali 103 kati yao
wavulana 57 na wasichana 46.
Aidha wilaya bado una changamoto kadhaa zikiwemo za upungifu
wa walimu 267 kati ya walimu 726 wanaohitajika katika shule hizo za sekondari
zenye walimu 459 wakiwemo wanaume 349 na wanawake 110.
No comments:
Post a Comment