Friday, March 25, 2011

MRADI WA YEBO YEBO HAUNA MASLAHI KWA WAMILIKI WA PIKIPIKI

Sintofahamu imewakumba vijana hawa walipo kutwa na gari la matangazo la Manispaa ya Songea kuwa wanatakiwa kulipia ushuru wa pikipiki za kukodisha ( yebo yebo ) katika manispaa shilingi 30,000 kila baada ya miezi sita.


Vijana hao walisema walizani kuwa kuendesha yebo yebo kungenusuru maisha yao kumbe imekuwa ni kuinusuru serikali kwa kukusanya ushuru kupitia yebo yebo hizo,walisema Mapato shilingi 95,000 kwa mwaka,BIMA shilingi 25,000 kwa mwaka na Halmashuri za Manispaa shilngi 30,000 kila miezi sita,bado polisi,matengnezo,mwenye pikipiki apate nini na dereva naye apate kitu gani ,je hiyo ndiyo ajira yenyewe?

KUUNDA KAMATI YA SEND OFF YA JESCA PAULO CHEMBELE SONGEA LEO

 leo ilikuwa ni siku ya hatua ya kwanza ya Bi Jesca Paulo Chembele ya kuunda kamati ya sherehe yake ya kumwaga.( Send Off) .Bwana Gaston na Bibi Chembele mwenye miwani na mama wa Bwana Gaston Chembele wa Namatui Songea wamewaalima wahisani wa kuwaunga mkono shughuli hiyo mhimu itakayo fanyika tarehe 23/6/2011.
 Hiyo ndiyo kamati tendaji ya sherehe hizo yenye viongozi watato akiwemo mwenye kiti,makamo mwenye kiti,katibu,makamo katibu na mweke hazina.katika ukumbi maarufu mjini hapa wa Songea Club.
Hawa ni wahisani waliokuja kuiunga mkono Familia ya Bwana na Bibi Gston Chembele wa Namatui Songea katika sherehe ya binti yao Mpendwa Jesca Paulo Chembele.Asilimia kubwa ya wahisani hao ni walimu.

USHURU WA WAENDESHA PIKIPIKI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA SASA UMEZIDI


Waendesha pikipiki kwa jina maarufu mjini hapa Songea Yebo yebo wameulalamikia uongozi wa Manispaa ya Songea kitendo cha kutangaza kuwa waendesha Yebo yebo walipe ushuru wa shilingi 30,000 baada ya miezi sita na siku ya tatu yake waanze kukamata wale wote wasio tekeleza agizo hilo.


Wandesha yebo yebo hizo wanasema wanalipa BIMA shilingi  25,000 kwa mwaka,TRA shiligi 95,000 kwa mwaka na kisha tena shilingi 30,000 kila baada ya miezi 6kwenye manispaa, wanasema hakuna faida yoyote kutokana na kuwa na utitiri wa yebo yebo katika manispaa hiyo.

Tuesday, March 22, 2011

LIKIZO NAYO INAPENDEZA UKIWA NA FAMILIA NYUMBANI BAADA YA KUTOKA KWENYE IBADA

 Dodoma baada ya kutoka kwenye ibada ya Kristmas mwaka jana tulipiga picha ya pamoja na mke wangu kama ukumbusho wa kumaliza mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011.
 Tukiwa ndani Binti yangu Sarah alitaka kutupiga picha ya wima kama tunavyoonekana na Mrs.
 Mrs Sikapundwa na wanae na mie nikawa Camera man niliwapiga picha hiyo wakati wakivywa vinywaji baridi .
 Sarah alipiga pisha kaka yake Michael  Siakapundwa  mwalimu Diploma mwaka wa kwanza yeye hakupenda kukaa kwenye mkeka wakati wa kula chakula unajua kula kwenye mkeka kunahitaji mazoea.
Bwana Joseph Sikapundwa yeye ni Diploma Chuo cha Biashara Dodoma ( CBE ) anaweza kukaa kwenye mkeka wakayti wa kula kama anavyo onekana akishambulia kipande cha nyama 
 Miea na mke wangu tulikaa kwenye mkeka ,lakini nilipata shida sana kwa kuwa ni shida sana,ilinipasa kugeuka geuka.
Hata hivyo inapendeza kukaa chini kwenye mkeka kukaa kwenye meza wakati wa kula ni utamaduni tuliouiga kwa wageni,Mapokeo ya kibantu kitu meza hakikuwaepo,Hivyo siku mojamoja si mbaya kukaa kwenye mkeka.

HABARI KWA UFUPI MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATIA SAINI UJENZI WA RELI

Mawaziri wa ujenzi kutoka nchi 3 za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Tanzania,Burundi na Rwanda wametia saini ya ujenzi wa reli ya pamoja ya Jumuiya hiyo.

BREAKING NEWS WATU 9,079 WAHOFIWA KUFA NCHINI JAPAN

Vifo vya waliokufa nchini Japan kutokana na tetemeko la ardhi na kufuatiwa na sunami vimeongezeka  kufikia zaidi ya watu 9,079 hadi sasa.

Monday, March 21, 2011

WAANDISHI NA WANATAALUMA WA HABARI RUVUMA HAWAUTAMBUI UONGOZI WA KIHUNI WA PRESS CLUB

 Mwenekiti wa Ruvuma Press Bwana Juma Nyumaya,leo ameweleza wandishi wa habari na wanataaluma wa habari kuwa yeye hana haja ya kugombania uongozi,ila kilicho takiwa ni taratibu katika kuchukua madaraka walio taka.Nyumayo alisikitika sana kwa kitendo kilicho fanywa na katibu mkuu wake wa Press club hiyo.



Aidha alisema yeye hajaajiriwa na Press club bali yeye ni afisa wa serikali ameajiriwa huko,sasa kwa nini wanamchafua? aliuliza,hivyo wao ni wasafi kiasi gani mapaka kuchuka hatu ya kupblish kwenye vyombo vya habari,kupeleka kesi polisi,kulikuwa na haraka gani,Ulikuwa ni uongozi huo tu ama kuna jambo.
 Baadhi ya wajumbe walichangia na kutafuta ufumbuzi wa mtafaruku huo,wote wamekubaliana kutoutambua uongozi huo wa watu walioshindwa kwenye udiwani.Bwana Stevin Mango yeye alichangia kuwa mkutano ufanyike tarehe 9/4/2011.

 Mwandishi mkongwe Bwana Komba Lipuka alisema jambo lililotokea ni jambo la aibu na la kihuni,maana haiwezekani waandishi wenyewe kwa wenyewe hawa aminiani je watu wengine watawaamini?
Bwana Adam Nindi mwandishi wa Star TV yeye alijaribu kusoma katuba ya nchi,na jinsi walivyo kratibu ziosea hao walifanya mapinduzi kwa kuwa walikuwa hawajui katiba ya nchi na katiba ya Club inasemaje kuhusu kiongoziakikose,



Wanachama na wanataaluma wa tasnia ya habari wa Press Club Ruvuma leo wamakataa kuwa katika uongozi wa kihuni ulifanywa na baadhi ya wanachama wa club hiyo kwa maslahi yao.kwa madai kuwa hawamtambui mwenyekiti wa Club hiyo Bwana Juma Nyumayo aliyechaguliwa kihalali.

Wamesema wao kama wana taaluma wa habari waliofundishwa maadili na miiko ya tasnia ya habari hawawezi kuongozwa na watu walioshindwa kwenye kinyang’anyiro cha udiwani na kukimbilia kwnye habari,kwani si chama cha waandishi wa habari bali chama cha wanasiasa waliotemwa na wananchi kwenye kata zao.

Hivyo chama cha madereva wa daladala mwenye kiti wao lazima awe dereva wa daladala na sio tingo,toka lini tingo alimwongozo dereva?.basi ni sawa na viongozi walioupindua uongozi wa Press club hiyo wakati yeye hayupo.

Aidha walisema mkutano mkuu utakuwa tarehe 9/4/2011 ambapo bwana Nyumayo atawakabidhi vifaa vya press ambavyo vinawafanya wakose raha,ila wale waandishi hawatakuwepo katika uongozi huo wa wanasiasa,wajiendeshe wenyewe tuone vipofu kwa vipofu wajionyeshe njia ya kupita.

Kibaya zaidi kilicho wakera waandishi hao ni Hatua ya taasisiya serikali ya chombo cha habari kutangaza habari za mwenye kiti huyo na kutaja tuhuma lukuki,bila ya kupata maelezo ya mtuhumiwa hayo, je hayo ndiyo maadili ya TBC.Kusema kuwa ni mbadhilifu,utawala wa mbavu,ikigundulika kuwa ni uzushi, akienda kukishitaki chombo hicho kwa kumchafulia jina lake,utu wake watakuwa tayari kujibia?

Ukweli hata waandishi wanashindwa kupata jibu,ni kweli Nyumayo alikuwa na uongozi wa kumabavu,au kuna kitu kinaenda chini kwa chini kati yake na hao wanao mwandama,maana licha ya kumchafua pia imemwathirika kisaikolojia.

HABARI KWA UFUPI WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA TUMBAKO MOROGORO WAFANYA KAZI KUBWA MSHAHARA MDOGO

Wanyakazi wa kiwanda cha tumbako mkoani morogoro wanaomba uongozi wa juu wa serikali kwenda kiwandani hapo,kusikia kilio cha wafanya kazi hao wanavyo fanya kazi kubwa lakini mshahara mdogo.kulingana na mfumuko wa bei ulivyo sasa.


Wanasema kuwa mshahara wanao pewa haufanani na kazi wanayo fanya.wanasema kuwa  kwa mwezi wanalipwa shilingi 87,000 tu.wakati tumabku ina matatizo mengi kiafya,walisema kuwa tumbaku ina sumu,lakini kutokana na ukosefu wa ajira ya kuaminika wameamua kufanya kazi kiwandani hapo.


Wanasema wanaomba Rais au Waziri mkuu kwenda kusikia kilio chao cha muda mrefu,kwani shilingi 87,000 ni kima kilicho pitwa na wakati, kwani mshahara wanao pata haulingani hata na mshahara wa kima cha chini serikalini

Sunday, March 20, 2011

DAGAAAAAAAA MWANZA NIMBOGA YA CHAPCHAP MKOANI RUVUMA NA NA MIKOA MINGINE TANZANIA

MAZIWA  ya Tanganyika,Victoria Nyasa nchini Tanzania ni maarufu sana kwa dagaa ambao wanapendwa sana na wanachi wake,Jumapili ya leo Blog hii imelikuta lori likipakua dagaa kutoka Mwanza Viwa Victoria Hapa mjini Songea.

NUANDA ZA JUU KUSINI NA KUSINI NDIYO MAZAO YA MAHINDI YAKO NAMNA HIIIIIIIIII

Hilo ni shamba la mahindi mkoani Iringa,Mbeya yako hivyo,Rukwa hivyo hivyo na Ruvuma ni vivyo hivyo,Serikali inaombwa kuwapa uwezo wakulima  katika pembejeo za kilimo ili mikoa hiyo iweze kuzalisha na ziada kwa ajili ya chakula cha wananchi wandani nawa nje.

MOROGORO KASORO BAHARI NA BAHARI INGEKUWEPO INGEKAUKA !! !

Hali ya hewa imeuathiri sana mkoa wa Morogoro,Morogoro ya leo si Morogoro ile ya mvua nyingi,milima ilikuwa ikitiririka maji,kwa ajili ya mvua nyingi,vyakula vilikuwa vya kumwaga ukianzia mahindi,mpunga,pamba na hata mtama vikiwemo viazi vitamu na mihogo.

Leo hii hakuna mvua ya uhakika katika mkoa huo,hazina ratiba ya kunyesha ya kuwafanya wakulima wajue ni lini wataanza kulima na kupanda.na ikinyesha siyo ya kuaminika inaweza ikakatika kabla ya mazao kukomaa.

HABARI KWA UFUPI MAREKANI,UINGEREZA NA UFARANSA ZAINGILI VITA VYA LIBYA

Imeripotiwa kuwa Marekeni ,Uingereza na Ufaransa zimeingilia kati vita ndani ya Libya na Waziri mkuu wa Uingereza  David Cameron alithibitisha kuwepo kwa ndege za kivita za nchi yake.

Saturday, March 19, 2011

MAMBO HAYA JAMANI YANAPENDEZA MATUMIZI YA MITANDAO IANZE NGALI WADOGO KAMA HUYO HAPO

SARAH Joseph ni mwanafunzi wa darasa la sita Martin Luther  primary school Dodoma,Huyo mwanafunzi unaweza ukasema maneno yoyote kwa lugha ya kiswahili ama kiingereza na yeye akaandika kwenye computer,huwa akirudi nyumbani anatumia computer kwa mazoezi zaidi.


Inapendeza iwapo vijana wetu wananza mapema kutumia computer wakiwa nyumbani kwa msaada wetu wazazi kama tunazo,ili akifika elimu ya juu asiwe mgeni wa vitu hivyo.

MAPROFESA WAKIANDIKA VITABU VYA ZIADA NA KIADA WIZARA YA ELIMU IVINUNUE

Rais Jakaya Kikwete  amewaomba wanataaluma,Maprofesa kutumia elimu yao kuandika vitabu vya ziada na kiada kwa shule za sekondari na za msingi ambako kuna uhaba mkubwa wa vitabu hivyo.

Niwa wajibu wa Wizara ya Elimu kuhakikisha vitabu hivyo vikiandikwa wizara ivinunue na kuvisambaza katika shule zake.Maprofesa wanacho sita labda ni ukosefu wa soko la kuuzia vitabu vyao maana kazi ni kubwa.Rais alisema hayo wakati alipofanya ziara makao makuu ya wizara ya elimu Dar es salaam.

JUMA MOSI YA LEO NA MATUKIO YA MAISHAAAA! WAZEEWETU WALIVYOISHI HADI LEO WAKO IMARA KABISA.

WAZEE wetu sijui walikuwa wanakula vyakula gani hapo zamani,Huyo mzee aliyeshika Bibilia ni mzee Dickson Bilali mkazi wa Mbalizi Mbeya tanzania umri ni zaidi ya miaka 80 lakini anasoma Bibilia na vipeperushi ya Yehova bila kuvaa miwani.na Creem bibilia na maandishi mengine.Mzee Bilal ni Baba mkwe wangu.


Mzee wa pili ni Mwinjilisti wa Mahsahidi wa Yehova Mzee Mwakasege wa Kanisa la Balizi,alimtembelea mzee Bilali nyumbani kwake kumtaka hali.Lakini cha ajabu siku hizi mtoto wa miaka 9 anavaa miwani ya kusomea Je hiyo ndiyo afya ya siku hizi za utanda wizi?.

Friday, March 18, 2011

BREAKING NEWS !!! JAPANI WATU 16,000 HAWAJULIKANI WALIKO AMA WAMEKUFA

INASEMAKANA  kuwa watu wapatao 16,000 nchini Japan wamehofiwa kufa au hawajulikani waliko kufuatia nchi hiyo kukumbu na janga la Sunami.

MBINGA MKOANI RUVUMA NA MIKAKATI YA KUINUA KIWANGO CHA TAALUMA NI JAMBO LA KUIGWA ?

 Wageni waliotembelea shule ya sekondari Nyoni Mbinga.

MIKAKATI walioweka ni kama ifoatavyo:-


  • kufundisha mada ngumu somo la hesabati
  • kubaini utoro kwa walimu na wanafunzi
  • kufanya ziara katika shule na ukaguzi
  • kujenga nyumba za walimu na vyamba.
  • kuhamasisha wananchi kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi.msingi na sekondari.

Thursday, March 17, 2011

BREAKING NEWS ! ! RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete asema kuwa waomi wandike vitabu vya kiada na ziada vitakavyo tumika katika shule nchini,Pia kusisitiza matumizi ya mfinzo kwa kutumia Internete ambapo somo litafundishwa wakati mmoja katika shule mbalimbali.Alisema hayo alipokuwa akiongea na wafanya kazi wa Wizara hiyo Jijini Dar
es salaam.



Wakati huohuo Rais amewataka wawekezaji wa kimataifa kuwekeza kwenye ujenzi wa reli.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa alimweleza Rais kikwete kuwa idadi ya watu wazima wasio jua kusoma,kuandika na kuhesabu inazidi kuongezeka.na kueleza mikakati mbalimbali ya kuweka mazingira ya elimu kuwa mazuri.


LOLIONDOOOO NA BARABARA ZINAKWAMISHA MAGARI YA WAGONJWA

 Hilo ni moja ya magari yanayo kodiwa na wagonjwa kwenda Loliondo kwa babu kutibiwa,unapewa kikombe kimoja tu kwa imani yako unapona.Babu anasema dawa hiyo ni ya kutibia na siyo ya kukinga.watu wote hao unaowaona wamesha kunywa dawa wako tayari kurudi kwao ila mvua ndiyo inaleta patashika.
Hawa ni wagonjwa ambao wamesha pata tiba,ila wanaomba serikali kuweka miundombinu ya barabara kuwa mizuri kwani walipata shida sana ya gari lao kukwama kwnye matope kwa ajili ya mvua zinazoendelea kunyesha kipindi hiki.

HABARI KWA UFUPI !!! BABU MCHUNGAJI LOLIONDO AONDOA HOFU WAGONJWA

LOLIONDO Arusha Tanzania,Mchungaji Asapwile ( Babu )
 anayetibu magonjwa sugu yaliyoshindikana Hospitalini,aondoa hofu kwa wagonjwa kuwa dawa ipo ya kutosha kwa watu wa ndani ya nchi na Nje ya nchi.

Aidha anasema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha ndizo zinazo fanya wagonjwa wakose raha wanapo safiri kwani magari mengi yanakwama kutokana na barabara kuwa mbaya.

WAFANYA KAZI TUJIFUNZE HAOOOO WAKIKUJNA MAGAZETI

Mafundi wa Tujifunze kusini wakiwa na hekaheka za kukunja magazeti na kuya hesabu wakati wengine wakiweka namba kwenye kazi nyingine zenye kuhitahi kuwekwa namba.

ELIMU HAINA MWISHO ELIMU YA WATU WAZIMA KITAIFA MAGUU MBINGA MAMBO YALIKUWA HIVI

 Kikundi cha MUKEJA cha uzalishaji mali cha Elimu ya Watu Wazima kijiji cha Kingerikiti Wilayani Mbinga wakicheza ngoma ya kioda siku ya kutembelea vikundi vya MUKEJA.
Kurugenzi wa Elimu ya Watu  Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Bwana Salum Mnjagila wa katika mwenye kaunda suti alitembele wilaya hiyo kabla ya maazimisho ya juma la elimu ya Watu Wazima Kitaifa mwaka jana Maguu Mbinga

MBINGA NA ELIMU YA SEKONDARI WALIVYO PANIA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUTOLEA ELIMU



 

Wilaya ya Mbinga imeweka  mikakati ya kuinua kiwango cha taaluma ya  elimu ya sekondari ambapo wilaya ina  shule za sekondari 60 kati yake shule 51 zinamilikiwa na serikali na Halmashauri, na 9 zinamilikiwa na mashirika ya dini na watu binafsi.

Kwa mujibu wa taarifa ya kutathmini elimu ya wilaya hiyo inaonyesha kuwa wilaya ina wanafunzi 23,140 kati yao wavulana 12,003 na wasichana 11,137.katika idadi hiyo wanafunzi walemavu wa aina mbalimbali 103 kati yao wavulana 57 na wasichana 46.

Aidha wilaya bado una changamoto kadhaa zikiwemo za upungifu wa walimu 267 kati ya walimu 726 wanaohitajika katika shule hizo za sekondari zenye walimu 459 wakiwemo wanaume 349 na wanawake 110.



HEKAHEKA ZA KUBORESHA ELIMU WILAYA YA MBINGA MKOA WA RUVUMA ZIMEPAMBA MOTO

Wanafunzi wa shule ya msingi walemavu Huruma Mbinga mjini wakiimba wimbo wa shule kwa wageni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walipo tembelea shuleni hapo mwaka jana.



Wilaya ya Mbinga  Mkoani Ruvuma yenye Tarafa 9 na kata 49 zilizotokana na kuongezeka kwa Tarafa tatu na kata 12 baada ya kuzaliwa Wilaya mpya ya Nyasa,ina shule za msingi 318 zenye wanafunzi 100,925 kati yao wavulana 50,498 na wasichana 50,527 ni wilaya yenye maendeleo mazuri kitaaluma na changamoto zake katika uboreshaji wa taaluma mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Tathmini ya elimu ya Mbinga na Mpango wa mwaka 2011 juu ya uboreshaji wa Taaluma inaonyesha kuwa wilaya ina upungufu wa walimu 424 sawa na uwiano wa 1: 40.kati ya walimu 2,159 waliopo.

Aidha mwaka 2010 wilaya ilipewa mgao wa walimu 22 ambao wote wamepangiwa shule zenya upungufu,sambamba na hilo watoto 12,259 wakiwemo wavulana 6,131 na wasichana 6,128 wameandikishwa  kuanza darasa la kwanza mwaka huu,kati ya watoto 16,216 kati yao wavulana 8,236 na wasichana 7,980 waliotarajiwa kuandikishwa shule.

WAGENI WATEMBELEA TUJIFUNZE KUTOKA CHUO KIKUU DODOMA (UDOM)

 Wageni wanaonyeshwa Blog ya TUJIFUNZE
Tujifunze imepata bahati ya kutembelewa na wageni kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM wa Idara ya Kiswahili Chuoni hapo.Wa katikati mwenye shati la maua ni Bwana Athumani S. Ponera wa Idara ya Kiswahili Dodoma,anaye mfuatia mwenye tai ni Bwana Isdory V. Nyoni mwenyeji wa Songea aliyeambatana naye na aliyekaa ni mwenyeji wa Tujifunzi Mhariri wa TUJIFUNZE Bwana Christian Sikapundwa.

Lengo ni kuja kuandaa mazingira ya kuwaleta wanachuo wao kwenye mafunzo ya uandishi na uhariri wa habari,vitabu na namna ya kutumia mitandao katika  habari.kama vile New Media Through Internet mf.Blogs,Facebook Twiter na mengine mengi watapata katika muda watako kuwepo hapa.

Wednesday, March 16, 2011

KIDATO CHA TANOOOOOO, MAJINA WAZIRI AYATANGAZA LEO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prf.Shukuru Kawambwa leo amatangaza majina ya wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano mwaka huu.

Waziri amesema mwaka huu kiwango cha kuingia kidato cha tano na watakao jiunga na vyuo vya ufundi imeongezeka,waliochukua sayansi,pia wamaeongezeka wakiwemo wasicha.waliokuwa wengi katika masomo ya sayansi jamii

Mazingira siyo rafiki mashuleni yanachangia kushuka kwa elimu

Hayo ni maoni ya taarifa ya mjumbe Bw.Joramu Mwaipopo wa kituo cha uchapaji  Kanda ya Kusini wa Tathmin ya Elimu ya Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika Peramiho.Alisema katika kikundi chao wamebaini mapungufu mengi yanayochangia kushuka kwa elimu,yakiwemo,nyufa katika baadhi ya madarasa,madawati haba.

Aidha Bw.Mwaipopo katoa rai kwa wadau wa elimu hao kuwa wakitumie kituo cha uchapaji kwa kuchapisha mitihani ya Mock ya darasa la saba,kidato cha pili,tatu,nne na sita.

Mvua imesababisha mazingira ya Manispaa ya Songea kuharibika

 Hiyo ni barabara  ya stand kuu karibu na Zahanati iliyo kuwa ya  Veris,ikielekea kwenye dumple la takataka ambayo inawapa shida madereva wanaokwenda kuzo taka hizo kwa lori.
Hilo ni Dumple lenyewe ambalo lipo chini ya barabara hiyo yenye mashimo sawa na mahandaki kwenye Manispaa hii ya songea.

Mnazi ni mmea wenye matumizi mengi

  • Shina la mmnazi hutumika kwa ujenzi wa vibanga na nyumba.
  • Kiungo cha mboga au chakula hasa wali.
  • Mafuta ya kupikia au mafuta ya nywele.
  • Vifuu hutumika kwa kutengeneza mapambo.
  • Kuni.
  • Majani kuezekea nyumba,vibanda,na mafagilio na hatimae,mitego ya samaki.

Monday, March 14, 2011

MBINU YA KUBORESHA ELIMU MTWARA YAFANIKIWA

Mkoa wa Mtwara umebuni mbinu ya kuboresha elimu kwa makato ya zao la korosho kwa wakulima,kwa mujibu wa taarifa ya Tathmini ya elimu RCC mkoani humo ,imesema kuwa wananchi wamehasika sana katika kuchangia elimu kupitia makato ya zao la korosho.

Hongera wananchi wa Mtwara,na wengine waige mfano huo katika kuboresha elimu katika mikoa ,wilaya zao.


LEO SIKU YA PAI DUNIANI

Wanafunzi wametakiwa kuhamsishwa kupenda hisabati,hisbati ni somo linalofundishwa kutokana na mazingira,somo hilo si gumu bali huwa wanafunzi wanakatishwa tamaa na wenzao,ama wao wenyewe wakijenga hofu kuwa ni gumu.

Wasichana wanaweza sana somo hilo,lakini imebainika kuwa baadhi ya wavulana wasiolipnda somo hilo wanawakatisha tamaa.

Somo hilo ni rahisi halihitaji kukariri,bali ni kuelewa kanuni na njia za kufanya hesabu,mwanzo walimu wa hisabati akiingia darasani Introduction yake ni kuuliza wanafunzi maswali mafupimafupi ya orodha au table 1 hadi 12hivyo ilimlazimu mwanafunzi kuziimba orodha kwa kichwa.

Na pai walimu wa somo hilo wanafundisha kwa nyimbo,na zipo kwenye CD mwenyekiti wa somo la hisabati ameandaa CD hizo ,hivyo walimu wa somo hilo wazinunue ili ziwasaidie katika kufundisha pai.

MATOKEO YA KILIMO KWANZA MKOANI RUVUMA MAHINDI YANALALIANA BOHARI YA KUHIDHAFI MAHINDI

Kilimo Kwanza imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa walanguzi wa mahindi waliokwenda kununua mahindi huko huko vijijini kwa bei ya hasara,kisha kuyauza kwa faida wakimwacha mkulima hana kitu.

Serikali imenunua mahindi hadi msimu wa kununu mahindi hayo umekwisha na mahindi bado wananchi wanayo vijijini,ambayo yanakutana na mahindi yaliyokuwepo shambani,hata kwenye hifadhi ya taifa Luhuwiko bado kuna mahindi ya mwaka juzi,mwaka jana na mengine  bado yako shamba.

Serikali iangalie uwezekano wa kuyasomba mahindi hayo wapelekewe wenye shida ya chakula,pia wakulima watafutiwe soko la kuuzia mahindi yao baada ya mavuno,kwani walanguzi bado wanawalalia wakulima.

HABARI KWA UFUPI ! ! ! MKOA WA RUVUMA WAFANYA TATHIMINI YA ELIMU KWA SIKU TATU

Mkoa wa Ruvuma umefanya tathimini ya elimu kufuatia kufanya vibaya katika mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne mwaka jana.

Tathmini hiyo ilifuatia na ziara katika shule za msingi na sekondari,kuangalia mazingira ya kutolea elimu,majengo ya shulie,madawati na walimu  waliopo katika shule hizo.


HABARI KWA UFUPI !!! TETEMEKO LA ARDHI LAATHIRI UZALISHAJI

Imeripotiwa kuwa, upatikanaji wa chakula na mafuta kwa ajili ya matumizi katika mji wa Sendai nchini Japan umeanza kuwa mgumu baada ya tetemeko la ardhi kuathiri uzalishaji.

Sunday, March 13, 2011

HABARI KWA UFUPI, SERIKALI YAMRUHUSU MCHUNGAJI LOLIONDO KUTIBIA WAGONJWA

Hatimaye serikali imemruhusu mchungaji Ambilikile Asapwile kuendelea kutoa huduma ya matibabu,baada ya kusimamishwa hapo awali na Wizara ya Afya na Ustwi wa Jamii.

Thursday, March 10, 2011

BREAKINGNEWS MAJESHI YA GADDAFI YA VAMIA MJI WAZAWIAYA

Ndege za kivita na vifaru vya wanajeshi wa  Gaddafi vyavamia mji wa Zawiya ambao kuna waasi wanaompinga Rais wa nchi hiyo.

Wednesday, March 9, 2011

HABARI KWA UFUPI WANAWAKE NCHINI UGANDA WANAFURAHA BILA KUPIGWA NA WAUME ZAO

Wakati  Dunia iliazimisha siku ya    wanawake kupinga unyanyasaji wa kijinsia,kukataa mifumo dume,lakini wanawake nchini Uganda wao hawana raha kama hawatapigwa na waume zao. Wanawake hao wanadai kuwa iwapo mme hatampiga mkewe,tena hata kuma kumtoa damu kwa kitu chenye ncha kali,wanadai kuwa wanaume kama hao si wanaume kamili.

Monday, March 7, 2011

MABANGO YA MATANGAZO YANACHANGIA KWA KIASI KIKUBWA MAPATO YA HALMASHAURI ZA JIJI,MANISPAA NA MIJI

Watu kadhaa wametoa maoni yao kuhusu tamko la serikali la kutaka kuondoa mabango kandokando ya baraba,kwa lengo la upanuzi wa barabara,na mabango mengine,katika Halmashuri za Jiji, Manispaa,na Miji kuwa ni zuri ,kwa maeneo ya barabara ambazo zinazotakiwa kupanuliwa au mabango ambayo ni machafu yaani hayana matunzo yabomolewe.

Bali mabango ambayo yapo matika maeneo ambayo hayahitaji kufanyiwa marekebisho yabakie,kwani yana ingiza mapato katika Halmashauri zetu nchini,pia yanasaidia kutangaza  biashara za watu,na watu wanarahisishiwa kujua vitu wanavyovitafuta kwa urahisi.

BREAKING NEWS ! Wafanyakazi 100 kuchangia damu

Wafanyakazi wa African Barrick Gold na Kampuni tofauti ziko Masaki wamechangia damu ili kuwasaidia wahanga wa mabomu ya Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam.

HABARI KWA UFUPI VIBANDA KATIKA MAENEO YA BARABARA VISIBOMOLEWE - PINDA

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda alisema kuwa Mheshimiwa Magufuli asitishe wito wake wa kubomoa vibanda  vilivyoko katika maeneo ya barabara.

Sunday, March 6, 2011

NI MAMBO YA DUNIA SAYARI YENYE UHAI KWA UUMBAJI WA MUNGU BINADAMU KAAMBULIA KUTENGENEZA VITU.

Dunia ni matokeo ya uumbaji wa Mungu,ambayo viumbe vyote vimo ndani yake,vyenye uhai na visivyo na uhai.Lakini kuna Tafsiri nyingi zilizotolewa na Maandiko mbalimbali ya vitabu vya Dini,na wanasayansi katika kuielazea Dunia.


DUNIA ni moja wapo ya sayari ambayo iliyokamatia uhai wa viumbe vyenye uhai na vitu visivyo na uhai.Na kubwa zaidi kuna binadamu ambaye aliambiwa na Mungu avitawale vitu vyote vilivyomo katika Dunia,kwa kuwa kapewa akili na utashi.

Kwenye ardhi viumbe hai ni vingi ambavyo tunaamini wanasanyansi wameshavibaisha kwa mamilioni yake, wanyama kwa makundi yake,ndege warukao na wale wasio na uwezo wa kuruka kutokana na uzito wao kama mbuni,kuna mimea,kuna miamba,kuna maji ambayo yameitwa bahari,mito,mabwawa,chemichemi.

Sifa za dunia kuwa na majira mbalimbali katika mwaka,kutokana na kuinama kwake kwa digrii 23.5.Hilo hufanya kuwe na viwango mbalimbali vya hali ya hewa joto au baridi.Mwinamo wake katika mhimili wake umeonekana kuwa bora kabisa,ili kuendeleza uhai.

Je ni kweli Dunia inamzingo wakilometa 40,000 na inazunguka mara moja kila saa 24.?
Je maeneo maeneo yaliyo kwenye Ikweta au karibu yanasonga kwa kilometa 1,600 hivi kwa saa?
Ni kweli Dunia inazunguka jua kwa kilometa 30 hivi kwa sekunde? Ambapo mfumo wa jua kwa ujumla unazunguka kitovu cha kilimia kwa mwendo wenye kustaajabisha kwa kilometa 249 kwa sekunde.Je unaweza kulinganisha na risasi inayosafiri kwa mwendo unaopungua kilomita mbili kwa sekunde?

Hayo mambo ya Sayari ambazo ni kazi ya Mungu,aliye umba mbigu na Dunia na ndani ya Dunia hiyo kaumba vumbe vyenye uhai na visivyo na uhai.Ambapo kamuumba Binadamu  atawale vitu hivyo vya nchi kavu na vya majini.Baadhi ya Binadamu hao ndio wanasayansi ,walijaribu kubuni vitu mbalimbali na wakaweza ila wakashindwa kumtengeneza binadamu mwenzao ambaye angefanana na wao,Unadhani kuna siku huyu binadamu anaweza kuumba binadamu mwenziwe?.

Saturday, March 5, 2011

WASANII NA VITUKO VYA WASANII HASA WA SARAKASI KATIKA MANISPAA YA DODOMA.


Vijana hawa wamekuwa vivutio kwa wakazi wa Manispaa ya Dodoma kwa mbwembwe zao wakiwa barabarani na gari lao la matangazo,hao wameva kitu kama viatu lakini vina vigurudumu ambavyo vinamfanya ateleze kama kwamba anakwenda kuanguka kumbeanateleza tu ila kwenye lami zaidi,wenzetu mchezo huo wanautumia kwenye theluji ( sliding ), pamoja na hao kuna wengine wanabaiskeli ambazo wanaziendesha kiufundi wa kiukweli,wanaweza kuruka na baiskeli hizo kwenye mitaro,Blog hii imeshuhudia vituko hivyo leo.

KUTANA NA VITUKO VYA KUTISHA NDANI YA ( NILITAFUNA WANANGU 10 )

Kitabu cha Irene Mwamfupe Ndauka ni kitabu kilichoandikwa kwa lengo la   kuelimisha jamii kuhusu uchawi na wachawi walivyo zagaa katika jamii aliyoiandikia kitabu hiki,lakini ni jamii nyingi za kiafrika zinaimani  imani za kishirikina  au  uchawi na kuchawia wengine.Ambao ni mbumbu katika sayansi ya kichawi.

Mtunzi wa hadithi katika kitabu hiki,mhusika mkuu amemjenga kama kweli ni mchawi,kwa kuanza kuua mkewe kwa lengo la kupata mavuno mengi ya miwa kwa kushawishiwa na jirani yake ambaye alikuwa mashuhuri kwa uchawi,baadaye akawa maarufu wa kula  nyama za watu,ndipo alipowatafuna watoto wake 10 mmoja hadi mwingine. Zaidi utayakuta ndani ya kitabu hiki ambacho kinasomwa ,Afrika Mashariki.

Thursday, March 3, 2011

HABARI KWA UFUPI CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI DODOMA KITOA SHILINGI 100,000 KUCHANGIA WALIOADHIRIKA NA MABOMU GONGO LA MBOTO

Kufuatia milipuko ya mabomu Gongo la Mboto Jijini Dares salaam kuleta madhara kwa wananchi kwa kupoteza maisha yao na wengine majeruhi na uharibifu wa mali kadhaa hivi karibuni,Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma wametoa shilingi 100,000 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tukio hilo la kutisha.

Kufuatia tukio hilo bado wananchi wanahitajika kutoa misaada zaidi kwa wahanga hao,huko Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.

BREAKINGNEWS ! ! ! TUZO KILI MUZIC KILA MSANII KUJINADI KIVYAKE

Wasanii walioteuliwa katika kushindana kwenye tuzo za kili Music,wako katika zoezi la upigaji kura,ambalo limeanza kwa kila msanii kujinadi kivyake.

MAMBO YA MAKAO MAKUU DODOMA KABLA YA KUINGIA STANDI YA DODOMA ,UTAPOKELEWA NA KEEP LEFT UKITOKEA DAR ES SALAAM

Ukitokea Kisasa katika Manispaa ya Dodoma kuelekea CBE,Jengo la Bunge utakutana na keep left hiyo ya kuvutia kwelikweli.kama unatokea Dar es salaam,unakaribishwa Makao Makuu Dodoma.hiyo kati ya keep left 4 zilizopo katika manispaa hii.

UBUNIFU WA VIJANA MJINI MOROGORO DUKA KATIKA BAISKELI

Wakati vijana wakihangaika namna ya kujikwamua kiuchumi baada ya kukosa ajira ya kuajiriwa katika ofisi mbalimbali ndani ya Serikali au katika taasisi binafsi,kijana huyu amebuni duka lake kwenye baiskeli yake ,ni machinga wa aina yake wa kuuza bidhaa hizo kwa ubunifu aliyotumia,kamera yetu ilimpata katika Standi ya mabasi mjini Morogoro.

Wednesday, March 2, 2011

MAWELE AU UWELE NI ZAO MOJAWAPO KATIKA MKOA WA DODOMA BLOGU HII LEO IMEUSHUHUDIA ULIVYO STAWI

Uwele ni zao linalo stawi maeneo yenye mvua kiasi au maeneo yenye ukame,Mkoa wa Dodoma ni mkoa wenye kustawi kila aina ya mimea ya chakula,yakiwemo mahindi tatizo mvua hunyesha na kuondoka,na kuyaacha mahindi bado kukomaa.

Ila mwaka mvua ikiwa nzuri mavuno yake si ya mchezo kama ilivyo Kibaigwa,Kongwa,Mpwapwa.Kongwa ndiyo inayotoa mazao ya mahindi kwa wingi na kuyapeleka Dar es salaam na nje ya nchi.

VIJANA NA HARAKATI ZA MAISHA MJINI MOROGORO,SASA WAMEAMUA KUJIAJIRI WENYEWE

Vijana hawa wanahekaheka ya kujikwamua kimaisha  wakiwa anapakua ndizi kutoka vijini Matombo na Mgeta baada ya kushushwa kwenye malori,kazi ni kazi mradi mkono uende kinywani.Vijana hawa wakipewa mikopo kupitia serikali zao za vijiji na mitaa wataleta maendeleo yao na ya taifa hili kwa ujumla.

RUZUKU IKITUMIKA VIZURI VITU VINAONEKANA KWA MACHO WALA SI MAJUNGU BLUGO HIIII IMEANZANIA MOROGORO HADI DODOMA.

 Hiyo ni keep left ya Manispaa ya Morogoro Masanvu jinsi inavyo onyesha usafi wa hali ya juu katika maeneo yake kabla ya kuingia standi kuu. 

Hapo chini inavyoonekana Keep  left hiyo nadhani ni mfano mzuri wa watendaji wangine waliopewa dhamana ya kusimamia miji yao.

MICHEZO !!!!! WANALIZOMBE WASONGEA ( MAJIMAJI ) LEO YATOKA SARE YA BAO MOJA NA AZAM KATIKA UWANJA WA UHURU WA DAR ES SALAAM

Tuesday, March 1, 2011

HABARI KWA UFUPI WATOTO 300 WAKAA CHINI KWA KUKOSA MADAWATI TUNDURU

Wazazi wakikosa mwamko wa elimu katika jamii mambo mengi yatakwama katika maendeleo ya elimu ya watoto nchini,Wazazi wa shule ya msingi na ufundi Mataka hawa taki kuhudhuria vikao,kutoa michango ya kununulia madawati.hawa ni baadhi ya wanafunzi 300 walokosa madawati shuleni hapo.

   SHULE ya msingi na ufundi Mataka iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma inakabiliwa na upungufu wa madawati 100 hali iliyosababisha wanafunzi 300 kukaa chini.
    Mwalimu mkuu wa shule hiyo Hassan Nakoma alisema hivi karibuni kuwa shule hiyo ina wanafunzi 768 kati yao wasichana 350 na wavulana 418 na kwamba idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la tatu na nne wanakaa chini.
    “Hali ni mbaya zaidi katika darasa la tatu ambalo lina madawati manne tu ambayo yanawezesha kukaa watoto wanne kila dawati hivyo  watoto wengi wanakaa chini,tumezungumza na wazazi  na kuwaita katika vikao hawafiki na wameshindwa kuchangia hadi sasa wazazi watatu tu ndiyo wametoa fedha sh,15,000 sawa na kununua madawati matatu tu,kamati ya shule ipo lakini  wazazi hawana mwamko katika elimu”,alisema.( source Albano Midelo Tunduru )
 

MAONI WA WANANCHI WALIO ONGEA NA BLOGU HII MJINI MOROGORO,RUVUMA NA MBEYA KWA WAKATI TOFAUTI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jaakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Wa - tanzania Mjini Dodoma.Pia alihutubia Bunge Jipya,na kama kawaida yake kuonge na wananchi kupita vyombo vya habari, wananchi wame toa maoni mengi sana kuhusu mstakabali wa  kujenga Taifa.

Wote hao hawakupenda majina yao yatajwe.Walisema mambo yafuatayo Rais ayaangalie kwa ukaribu:-
  • Kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa mbambali zikiwemo vyakula,vifaa vya ujenzi na vitu vingi wameviainisha katika maoni yao.
  • kero za vijana na hatima yao,wapewe mikopo ipitie ngazi za chini kwenye serikali za vijiji na mitaa,kisha ifuatiliwe Isiwe kama faidika  na mapesa ya kikwete kupitia Benki ya NMB.walinufaika wajanja wachache wenye dhiki walizisikia redioni.
  • Rais awe mkali kwa mambo yanayo tekelezwa na watendaji wake bila viwango kwa jina jinine kuchakachuliwa.Asiwaone haya wanavuruga mipangilio aliyoiweka kwa ajili ya kumletea mwananchi maendeleo.Asiwachekee wanaotaka kuvuruga wananchi kwa kutumia maandamano yenye picha za kisiasa ndani yake.
  • Watendaji wasio kidhi viwango waondolewe madarakani awateuliwe wengine kulinda heshima ya nchi na Taifa kwa uju,mla.
  • Matendo yawe mengi zaidi kuliko maneno katika ngazi zote za uongozi.Na Rais afuatilie ili kudhibiti mianya ya uzembe kwa watendaji wake ,akifanya hivyo kutaondoa hata maswali tata kutoka vyama pinzani..kwani wapinzani  wao hawaoni hata moja jema lililo fanywa na Chama Tawala tangu Uhuru.