Friday, May 11, 2012

ULINZI SHIRIKISHI WA WANANCHI NA POLISI KATA NI MUHIMU KWA USALAMA WA RAIA NA MALIZAO,WANANCHI WAUNGE MKONO FALSAFA HIYO - GEORGE CHIPOSI

 Kaimu kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma George Chiposi awashukuru wananchi wa Kata ya Mshangano leo kwa kuanzisha ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii.Aidha kamanda Chiposi amewataka wananchi kushirikiana na Polisi katika ulinzi wa Raia na malizao katika maeneo yao wanayoishi.Pia amaomba oungozi wa Jeshi la Polisi Makao makuu Dar es Salaam kuwa patia vitendea kazi vikiwemo magari kwa ajili ya doria wa ulizi shirikishi katika mitaa.
Bwana Kibwana Dachi mwenye tai akiandaa kipindi cha Mtandao wa Dawati la Polisi wanawake katika Jengo la Mtandao huo katika Kituo cha Polisi Songea Mjini leo.
Mwenye kiti wa Ujenzi wa jengo la Dawati la Polisi wanawake  pia ni mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Songea Mjini Inspector Anna Tembo akielezea mafanikio na manu faa yatakayo patikana baada ya jengo hilo kikamilika.Aidha amewashukuru wadau waliyoguswa kuchangia fedha katika ujenzi huo,pia kawashukuru wanahabari wakiwemo Bw.Juma Nyumayo na Adam Nindi ambao walishughulikia katika harambee ya kuchangisha fedha na kusimamia ujenzi wa Jengo hilo.
Inspector Anna Tembo akisaini kitabu cha wageni katika jengo hilo leo katika Kituo cha Polisi Songea Mjini.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma George Chiposi alikisalimiana na viongozi wa kata ya Mshangano Halmashauri ya Manispaa ya Songea leo kabla ya kuongea na baadhi ya ulinzi shirikishi wa kata hiyo.
Bwana Adam Nindi  mwenye koti Mdau na msimamizi wa harambee ya fedha za ujenzi wa jengo hilo.Alesema watu wenye uchungu wa kuzaliwa na mwanamke wameguswa na kuchangia milioni 10 laki tano na wanaendelea kuchangia hadi milioni 32,Natu wadiniwameguswa na mtandao huo ambao utasaidia kupunguza uhalifu na unyanyaswaji mbalimbali.Aidha alisema katika shughuli hizo hawakushirikisha wanasiasa wala watu wanaopenda kujaza matumbo yao.
Naye Bw.Juma Nyumayo anaelezea umuhimu wa kuwa na jengo hilo ambalo amesema kupitia jengo hilo watu watajifunza,madhara ya udhalilishaji kijinsia wanawake na watoto,pia hata kuna baadhi ya wanaume wananyanyaswa na wake zao.yeye ni mmoja aliyeshiri katika kuhakikisha fedha zinapatikana na kuwasimamia mafundi hadi kufikia hatua ya kuweka jiwe la msingi.
Bw.Nyumayo akiwa na wageni kutoka makao makuu ya Polisi Jijini Dar es salaam na waandishi wa Channel Ten leo katika kituo cha Mtandao huo wa Polisi wanawake katika Manispaa ya Songea.


TIMU YA MAAFISA  WA POLISI  KUTOKA DAR ES SALAAM  NA WAANDISHI WA HABARI TOKA CHANNEL TEN  DAR ES SALAAM KUTEMBELE  DAWATI LA  MTANDAO  WA  POLISI WANAWAKE SONGEA LEO

Katika msafala huo umehusisha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Patrick Massawe, KoploVigilius Lundera ,Konstebo Hassan Mndeme, Kibwana Dachi mwandishi wa habari toka Channel Ten na Moses Masenga pia wa Channel Ten kwa lengo la kurekodi vipindi vya kuhamasisha Polisi Jamii kuhusu ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na Polisi Jamii akatika maeneo yao.
   Bwana Kibwana Dachi msimamizi wa Vipindi Vya Channel Ten katika kurekodi vipindi hiyo alisema wameanzia mkoa wa Mbeya wakafika Mkoa mpya wa  Njombe kwa shughuli kama hizo,lakini  katika Dawati la mtandao wa Polisi wanawake hawaja kuta jengo la dawati mtandao kama lilivyo Jengo la Dawati la Polisi wanawake katika Halmashauri ya Songea.
   Ambapo mwenyekiti wa ujenzi wa jengo hilo  Inspector wa Polisi, pia ni kuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Songea Inspector Anna Tembo,ambaye amewashukuru wadau wa mtandao huo ambao wameguswa na kuamua kuchangia fedha na vifaa vya ujenzi wa jengo hilo la kisasa ambalo limewekwa jiwe la msingi wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment