Wednesday, May 2, 2012

HAKUNA MABADILIKO YA MTAALA WA ELIMU ,ILA KUNA MABORESHO YA MTAALA HUO – DKT MUSHI

 Dkt Mushi akielezea Tafakuri ya maboresho ya mitaala na mkakati wa mafunzo kwa wadau,katika ukumbi wa Maliasili Songea Ruruma jana kwenye mafunzo kwa wadau wa elimu mkoani humo.
 Afiaslimu Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo akimtambulisha wadau wa elimu kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania wa kwanza kushoto kabla ya kuanza mafunzo hapo jana katika ukumbi wa Maliasili Songea.
 Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul Mushi wakwanza kushoto.
Picha ya pamoja ya pili ambapo nami nikiwemo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Mushi wa katikati yangu.


MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul S,D.Mushi alisema hayo kwenye semina ya kazi kwa wadau wa elimu wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma zilizo jumuisha Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri,Makatibu tawala wa Wilaya,maafisaelimu,wakaguzi wa shule,katika ukumbi wa Maliasili Songea jana.

Dkt Mushi alisema kuwa watu waache imani potofu kuwa elimu inadorora kwa sababu ya mitaala ya elimu inabadilika kila mara,siyo kweli isipokuwa kuna maboresho ya mtaala ambapo imeboreshwa siyo zaidi ya mara 5 katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.
   Aidha Dkt Mushi alisema Taasisi ya elimu imeweka mikakati ya kuinua elimu ili kuijenga nchi,kwa njia shirikishi kuanzia ngazi ya chini kabisa kwa lengo la kuwajengea watoto wamalizapo elimu ya msingi wajue kusoma,kuandika na kuhesabu (kkk).
Alisema wadau wa elimu wakiwa na mkakati wa kujenga stadi za msingi za kkk,nao watumia vikao katika wilaya na Halmashauri zao,na halmashauri hizo zitatumia midahalo ya wazi,katika ngazi zote,kaya,shule,Tarafa,Wilaya,Mkoa,Kanda hadi Taifa.
Alisema watu waguswe kwa pamoja sio kulaumiana na kunung’unika na kumtafuta mchawi kuhusu changamoto za elimu,bali kila mmoja kujipima binafsi jinsi anavyoweza kuwajibika  kila mdau ana wajibu wa kuguza hali ya mdondoko wa elimu nchini.
   Wakati huo huo wadau wa mafunzo hayo wamemhakikishia kuwa changamoto zote zilizoainishwa katika mafunzo hayo yatatekelezwa kwa kila Halmashuri ili kuondoa kero ya kkk kwa wanafunzi kutokana na hoja walizoziibua kwenye makundi ya majadiliano kwa kila Halmashauri.
    Baada ya majadiliano hayo kila wilaya ilitoa haoja walizoziibua ambapo Tunduru ilitolewa na Mwalimu Luya Ngonyani ( katibu wa CWT Mkoa wa Ruvuma),Manispaa na Songea Vijijini ilitolewa na Enea Mpogole Afisa elimu Vielelezo,Mbinga ilisomwa na Idd Alimbe  Mponda ( DAS Mbinga ) na Namtumbo ilitolewa na Sekela Mwamwezi Mkaguzi mkuu wa shule wa Wilaya.
   Leo Dkt Mushi ataelekea Jijini Mbeya kwa mafunzo kama hayo,hatimaye Mtwara Lindi kwa shughuli kama hizohizo.

No comments:

Post a Comment