Sunday, May 6, 2012

TAFAKURI YA JUMAPILI LEO,'MIMI NI MZABIBU WA KWELI NA BABA YANGU NI MKULIMA'

 PADRE Aluwen Otieno akipokea vipaji katika ibada ya kwanza katika kanisa kuu la Songea mjini leo,kwaya iliyo imba katika Ibada hiyo ni kutoka Madaba Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.


Padre Aluwen Otieno Paroko msaidizi wa kanisa kuku la Mtakatifu Mathias Mlumba Kalemba la Mjini Songea,alisema hayo katika mahubiri yake kwa waumini katika Ibada ya kwanza.”Alisema kuwa Yesu  aliwaambia wafuasi wake kuwa ,Mimi ndimi Mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima  na kila tawi ndani yangu lisilo zaa huliondoa  na tawi lizaalo hulisafisha’alisema
.
Nakwamba alisema mimi ni mzabibu ,nanyi ni matawi yangu akaaye ndani yangu nami ndani yake huyo huzaa sana,maana bila mimi ninyi hamuwezi kufanya neon lolote.Padre Otieno alisema mzabibu mbaya kuzaa matunda machachu na huo haufai,.

Alisema binadamu kwa tabia yake hupenda vitu vizuri , vibaya huvikataa na kuvidharau,lakini mtu katika jamii akiwa anafanya mambo mazuri pengine kwa manufaa ya jamii na taifa lake ,mtu huyo hatapendwa, watamlaumu,watamsengenya na kusema anajisumbua kazi hizi zinapita,walikuwa watu ,sembuse yeye tutamuona si tupo hapa.

Nakwamba hao ndiyo mzabibu mbaya unazaa matunda machachu ya chuki zisizo na maendeleo katika taifa lolote,alisema watu wakweli,watenda haki,waadilifu hawapendwi katika jamii ila wale ambao hawajali maisha ya wenzao jamii inawapenda,Binadamu anamsifia mwenzake kwa nje lakini ndani ya moyo wake anachuki,hayo ni matunda machachu ya mzabibu.

No comments:

Post a Comment