Gharama hiyo yenye mchanganuo
wa uchangiaji wa gharama za miradi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:-
- Nguvu za wananchi Tshs.296,022,645/=
- Halmashauri za wilaya na Manispaa Tshs.204,486,125/=
- Serikali Kuu Tshs.773,599,581
- Wadau wa Maendeleo Tshs.458,809,551/=
- Watu Binafsi Tshs.287,440,000/=
Mwenge uko Mkoani
Ruvuma Umepokelewa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma kutoka Mkoa wa
Njombe katika Wilaya ya Nyasa na kuanza
kukimbizwa katika wilaya zote tano zenye Halmashauri sita ambazo ni Wilaya ya Nyasa,
Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru.
Ukiwa Mkoani Ruvuma Mwenge wa Uhuru
utafanya kazi ya kufungua miradi 13 yenye thamani ya Tshs.390,684,832
kuweka mawe ya msingi miradi 22 yenye thamani ya Tshs.1,303,187,695,
kuzindua miradi 12 yenye thamani ya Tshs.141,045,375 na miradi 04
yenye thamani ya Tshs.34,840,000 itakaguliwa na kufanya jumla ya miradi
yote kuwa 51 yenye thamani ya Tshs.1,930,357,902.
Baba wa Taifa
mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema “Sisi tunataka kuwasha Mwenge na
kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini
pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima
palipojaa dharau”.
Mwenge umekuwa ni
kichocheo kikubwa cha shughuli za maendeleo, umoja, mshikamano na amani
kwa Taifa letu.Lakini usemi wa Baba wa Taifa unaanza kuingia dosari Amani hiyo
inaanza kutoweka,unasikia wenzetu Zanzibar Makanisa yanachomwa,tatizo hawataki
Muungano sasa kukataa Mungano kuna uhusiano gani na Kuchoma makanisa ?
Tunaelekea wapi sasa.
No comments:
Post a Comment