Thursday, May 17, 2012

MWAMBUNGU AWAMBIA WAKUU WA WILAYA KUFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI,WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA WANATEGEMEA KILIMO KWA MAISHA YAO,SASA DHAMANA KUBWA WAMEPEWA KUONGEZA MAENDELEO ZAIDI

 Mwambungu 'asema mmekabidhiwa dhamana kwenye wilaya zenu,wananchi wanategemea sana ushirikiano wenu katika kuendeleza maendeleo,Mkoa huu unategemea sana kilimo,hivyo wananchi wanategemea pembejeo za kilimo ,isitoshe mkoa una vyanzo vingi vya uchumi vyote vitategemea dhamana mliyopewa'
Aidha alisema kuwa mkoa huo uko nyuma katika elimu,hivyo dhamana waliyo pewa watajitahidi kuwa kushirikiana na sekta ya elimu na wananchi katika kuinua taaluma, alisema wafanye kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na kutekeleza kanuni za Ilani ya Chama  ( CCM ).Leo ameapisha wakuu wa wilaya watano ambao ni wa Wilaya ya Nyasana Ernest N Kahindi,Namtumbo Abdula Suileman,Songea Joseph Joseph Mkirikiti,Mbinga Senyi Simon Ngaga na Tunduru Chande Bakari Nalicho.
Picha ya pamoja na viongozi Mbalimbali Mkoani
 Picha ya pamoja na mataji wakuu hao wa wilaya na Mkuu wa mkaoa
Picha ya pamoja ya ukumbusho wao bila mataji.Kati yao Mama mmoja , wananchi wa mkoa wa Ruvuma wanawategemea sana katika kilimo,kupata soko bila ubabaishaji.

No comments:

Post a Comment