Sunday, May 27, 2012

MAUAJI YA WASICHANA KATIKA MANISPAA YA SONGEA YANAANZA KUREJEA TENA BAADA YA UTULIVU ULIYO PATIKANA BAADA YA MACHAFUKO YALIYOTOKEA KATIKA MJI WA SONGEA.

Msichana wa ambaye jina lake halikutambulika kupitia blog hii mkazi wa Mombambili ambaye alikuwa mamantilie amekutwa amekufa Jirani na Kambi ya JWTZ Ruhuwiko inasemekana kifo chake kilihusishwa na mambo ya kimapenzi.Inaelekea alichukuliwa na Mvulana toka Mombambili hadi Ruhuwiko Manispaa ya Songea,kisha kufanyiwa vitendo vibaya na kuuwawa na kutupwa kwenye mpenyo wa nyumba inayotarajiwa kuwa nyumba ya kulala wageni Polisi wanaendelea na uchunguzi uliyosababisha kifo hicho.
Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma ulikuwa shwari na kurejesha amani,sasa wimbi la mauaji linataka kurudia tena,sijui tatizo liko wapi,watu kuua watu wenzao hawaoni shaka,wala mwili kusisimka,amakweli shetani ananguvu,ni muhimu kukemea matukio hayo maovu,

No comments:

Post a Comment