Saturday, May 12, 2012

SIKU YA WAUGUZI DUNIANI,KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA SONGEA WAUGUZI WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZINAZO FANYA WASHINDWE KUTIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO.

 Maandamano ya wauguzi wa hospitali ya mkoa ya Songea wakielekea kwenye viwanja vya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo watapata nasaha kutoka kwa mgeni rasmi wa siku ya muuguzi duniani.
Wauguzi hao wanakabiliwa na changamoto kadhaa zinazofanya wasitekeleze kazi yao ngumu kama inavyo takiwa,lakini kutokana na changamoto hizo wauguzi hao bado wanafanya kazi yao kadri wanavyo weza za kuhudumia wagonjwa.
Muuguzi Mama Mbano alisema kuwa changamoto kubwa zinazowakabili ni pamoja na .Ukosefu wa vitendea kazi na kama vipo havitoshelezi kulingana na idadi ya wagonjwa wanavyo fika kutibiwa katika hospitali hiyo.Nyingine ni upungufu wa madawa,hazitoshelezi mahitaji ya wagonjwa ikizingatiwa Songea hospitali ni hospitali ya Mkoa. pia na upungufu wa wauguzi ,hawatoshelezi  ukilinganisha na ukubwa wa hospitali hiyo.

1 comment:

  1. Kwa hiyo kichotakiwa ni kwamba vitenda kazi viongezeke, madawa na wauguzi...Hata hivyo nawaongeza wauguzi kwa kazi waifanyayo

    ReplyDelete