Sunday, May 13, 2012

HONGEARA REO RUVUMA KUWA MKURUGENZI WA SEKONDARI,BIBI PAULINA MKONONGO MATUNDA YA KAZI YAKE YAMEJIONYESHA ,AENDELEE HIVYO KATIKA NAFASI HIYO

 Afisaelimu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa sekondari.Bibi Mkonongo anastahili kabisa kupata nafasi hiyo kutokana na kazi zake za ufuatiaji wa taaluma katika mkoa huo.Anauchungu na jamii inayohitaji kuelimishwa kwa uhakika,pamoja na changamoto nyingi zilizopo kwenye Sekta ya elimu.Tunamtakia kazi njema huko aendako.
Bibi Mkonongo wa kwanza kulia akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul Mushi watatu kushoto na wa katikati ni kaimu RAS Mkoani Ruvuma Injinia Tossi,kwa wadau wa elimu katika ukumbi wa maliasili mkoa Mjini Songea hivi karibuni.Kwenye kikao cha kazi kuhusu mitaala ya elimu.

Ambapo Dkt Mushi alifafanua kiundani kuhusu imani potofu ya baadhi ya wananchi kulaumu kuwa elimu inashuka kutokana na mabadiliko ya mitaala ya elimu kila kukicha.Alisema si kweli bali kuna maboresho ya mitaala hiyo.

No comments:

Post a Comment