MAWAZIRI
waliyo wajibika kutokana na utendaji mbovu wa majukumu yao,hawawezi
kuwajibishwa peke yao,ni pamoja na watendaji wao wakiwemo makatibu wakuu
wao,wakurugenzi,viongozi wa mashirika ya Umma kama wamo katika mkumbo huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete alisema hayo kwa wananchi kupitia vyombo vya habari Ikulu Jijini
Dar es salaam jana kabla ya kutangaza
Baraza lake jipya la mawaziri.
Alesema
inawezeka kuna baadhi ya Mawaziri hakuhusika na lolote ila ni kwa sababu ya
watendaji wao kwa lengo kukomoana,havyo vitendo hivyo haviwezi kuvumilika ni
budi na wao wahusike kwa hili.
Kwa
maoni mbali mbali ya wakazi wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamemsifia sana
Rais Kikwete kwa uamuzi aliyo uchukua wa kubadilisha mawaziri na wengine wapya
kuingia na wabovu kutolewa,hiyo ndiyo Demokrasi walisema watoa maoni hao,’Ni
baraza safi kama watatekeleza yale watakayo agizwa’.walisema.( Source TBC )
No comments:
Post a Comment