Friday, May 4, 2012

NIDHAMU CHUO CHA UALIMU SONGEA SASA NI SAFI ,KUMETULIA

Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Songea Bwana Ubaya Salum ,amesema kuwa hali ya utulivu katika chuo chake sasa ni tulivu.baada ya baadhi ya wanachuo waliyo sababisha vurugu chuoni hapo kutimuliwa.

Mkuu huyo wa Chuo alisema hayo jana alipotembelea katika ofisi ya TUJIFUNZE kuwa nidhamu imerejea kama mwanzo ambapo hapo awali wakufunzi wa chuo hicho waligoma kuingia madarazani kufundisha kwa kutolipwa mafao yao.Pia alisema na wanachuo nao baadhi yao walifanya fujo na walitimuliwa kwa maamuzi ya uongozi wa chuo hicho.

No comments:

Post a Comment