Friday, May 11, 2012

Polisi Jamii Kata ya Mshangano imepunguza kwa kiasi kikubwa vitendo viovu walivyokuwa wakifanya vijana kata hiyo.


 Kamanda mkuu wa usalama kata ya Mshangano Bwana Wolfugang,anasema kuwa kuna vikundi viwili vya ulinzi shirikishi cha kwanza ni cha ulunzi jamii na cha pili ni cha sungusungu ambavyo vinalinda usiku na mchana.anasema tandu zoezi hilo la ulinzi lianze vitendo vya wizi wa mifugo,uvutaji wa bangi kwa vijana vimepungua sana.
 Kikundi cha Lizombe kilitumbuiza katika hafla fupi ya kurekodi kipindi cha ulinzi shirikishi,Polisi Jamii Kata ya Mshangano leo.
 Inspector Paul Mashimbo anasema kazi ya polisi ni kutoa taaluma kwa wananchi maana kazi ya ulinzi ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi katika sehemu yake,maana ulinzi na usalama siyo kazi ya askari polisi peke yao. alisema hayo katika mahojiano na Channel Ten Mshangano Manispaa ya Songea leo.
 Inspector Paul Mashimbo akisalimiana na viongozi wa Kata ya Mshangano wakiwemo Watendaji wa kata za Mshangano,Msamala,na Shule ya Tanga.
RTO  wa usalama Barabarani ambaye ni mlezi wa Ulinzi na usalama Kata ya Mshangano,anasema kuwa ulinzi ni jukumu la kila mwananchi wakishirikiana na Polisi kata ili kudhubiti uhalifu unaotokana na jamii kuvunja maadili.pomoja na usalama wa raia na mali zao.

No comments:

Post a Comment