Sunday, May 27, 2012

JUMAPILI YA SIKUKUU YA PENTEKOSTE ,MITUME WALISHUSHIWA ROHO MTAKATIFU

Ilipofikiam siku hamsini baada cha kifo chake Yesu Kristo,aliwatokea mitume wake waliyojifungia ndani kwa kukata tamaa,kwani waliyemtegemea aliuawa.
Basi walishushiwa Roho Mtakatifu kwa ishara ya ndimi za moto,nakuwaambia kuwa mtakao waondolea dhambi wataondolewa na mtakao wafungia dhambi watafungiwa.Roho mtakatifu inatia nguvu,inaleta amani,nyumba isiyo na Roho mtakati haina amani,Ofisi isiyo na Roho mtakatifu haina mshikamano wa kuleta maelewano ndani ya kazi,
Ukosefu wa Roho Mtakatifu Katika Mataifa ndiyo sababu ya mahangaiko ya maisha,amani hakuna,uaminifu uanapungua,chuki,dharau,unyanyasaji,dhuluma ukiukwaji wa haki za binadamu unatawala katika mataifa mengi,Serikali ni watu ,na watu hao wakikosaka nguvu ya Roho Mtakatifu wananchi wake watahangaika,kwa manung'uniko ya hapa na pale kwa kukosa mahitaji yao muhimu ambayo walitegemea serikali yao iwatekelezee.Hivyo Jumapili ya leo ni ya Muhimu sana kwetu binadamu.Nawatakia Jumapili inayomalizika njema.'Amani na iwe kwenu' Aliwaambia Mitume wake ambo walikosa Amani.

No comments:

Post a Comment