Thursday, May 31, 2012

MTOTO ACHOMWA MIKONO YAKE MOTO NA MAMA YAKE WILAYANI KILWA KWA WIZI WA BOGA,MAMA AONYA WANAWAKE WENZAKE WASIWE WAKATILI KAMA ALIVYO MFANYIA MTOTO WAKE

Mtoto huyo ambaye jina lake halikupatikana katika Blog hii kama anavyoonekana kwenye picha hafifu lakini mikono yake inaonekana ilivyo fungwa bandeji,ni mkasa aliyoupata kutokana na kuiba boga aliloliweka mama yake mzazi kuliiba ndipo alipochomwa moto mikono yake.Mama yake akamficha ndani huko wilayani Kilwa Mkoani Lindi.
Ni ukatili wa aina yake wa kumchoma mtoto mikono kwa moto ati kaiba boga kweli huo ni uungwana ? kwa wanawake ambao ni mama zetu ?.Kilema ambacho hata kisahau cha kuchomwa na mama yake moto eti kaiba boga,itamwingia akilini kweli.Sasa wana Blog wenzangu hebu tulipembue kwa undani tukio hilo.



MAPENZI YA SABABISHA MTOTO MLEMAVU KUAWA NA KUTUPWA MTONI SONGEA

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma ( RPC ) Michael Kamuhanda anayehamia Mkoa wa Iringa baada ya kuongea na waandishi wa habari mkoani hapa leo katika kumtambulishi Kamanda mgeni wa mkoa huo ( RPC ) aliyehamishiwa hivi karibuni ACP Deusdedit Nsemike hayupo pichani..

MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu auawa na bwana wa mama mwenye mtoto Rebeka Cheni na kutupwa mtoni,Kamanda wa Mkoa wa Ruvuma anaehamia mkoa wa Iringa  Michael Kamuhanda leo amewaambia waandihi wa habari kuwa chanzo ya mauaji ya mtoto huyo ni mapenzi.
Alisema kuwa inasemekana kuwa mama wa mtoto huyo aliambiwa na bwana ambaye hakuzaa naye mtoto huyo kuwa wamuue ili waendelee na mapenzi yao kwa raha kwani mtoto huyo alikuwa mlemavu wa akili Tahira,ndipo mama huyo alivyo toka nje na kumwacha mwanae ndani,muda huo bwana huyo mkatili alivyo pata mwanya wa kummaliza mtoto Rebeka.
 Alisema baada ya kufanya kitendo hicho watuhumiwa walichukua mwili wa mtoto huyo na kuitupa mtoni,wasamaria weme walivyo kundua hilo waliitaarifu polisi.Na kwamba wote wako mikononi mwa polisi na upelelezi unaendelea.

KAMANDA WA POLISI ( RPC ) MGENI ACP DEUSDEDITH NSEMIKE MKOANI RUVUMA ATABULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO.NA AKAMANDA WA ZAMANI ANAYE HAMISHIWA MKOANI INGA MICHAEL KAMUHANDA

 Kamanda mgeni wa polisi RPC Mkoani Ruvuma ACP  Deusdedit Nsemike  baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma leo

 picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Ruvuma leo baada ya utambulisho wa RPC Mgeni nje ya jengo la polisi mkoa mjini Songea Kamanda mgeni  Deusdedit Nsemike wa tatu kutoka kushoto.

Bwana Juma Nyuamayo wakizungumza na rpc Michael Kamuhanda leo.
.
KAMANDA wa Polisi (RPC) Mgeni ACP Deusdedith Nsemike Leo ametambuliwa kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa Jengo la Polisi mkoani na Kamanda Michael Kamuhanda anaye hamishiwa mkoa wa Iringa.
  Kamanda Nsemike alisema kuwa atakuwa tayari kufanya kazi na waandishi wa habari,kwani nimuwazi,na kwamba anaomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa waandishi hao japo watapata jambo ambalo ni la uhalifu.
  Aidha alisema kuwa atahitaji utii  wa sheria bila masharti,Mahusiano pamoja na Idara nyingine zikiwemo za Ustawi wa jamii,Elimu,Afya ,michezo na Halmashauri za Wilaya.
  Vilevile alisema kuwa atahitaji ushirikiano na viongozi wa ulinzi na usalama ili kuhakikisha Falsafa ya Polisi Jamii inatekelezwa kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia sheria za nchi.
   Alisema kuwa iwapo wananchi watapata taarifa za fujo,ujambazi,zitaarifiwe mapema katika vyombo vinavyohusika kabla hakujatokea madhara makubwa.
Awali kamanda Michael Kamuhanda aliwaonba waandishi wa habari hao kuwa na ushirikiano wa karibu na Kamanda Nsemike kama vile alivyopata ushirikiano yeye katika kufanikisha shughuli zake za ulinzi na usalama katika Mkoa wa Ruvuma.
Pia akamweleza Kamanda huyo mgeni Mkoani hapa kuwa asiwe na mashaka na waandishi wa mkoa huo katika utendaji wao wa kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma Michael Kamuhanda amepata uhamisho kwenda Mkoa wa Iringa, Ni matumaini ya waandishi wa Mkoa wa Iringa watampa ushirikiano wa kutosha Kamuhanda katika shughuli zake,kwani wanahabari ni kioo cha Jamii

Tuesday, May 29, 2012

MADWA YA KULEVYWA NAYO NI HATARIII,BW,JUMA NYUMAYO ANAWAHOJI VIJANA WANAOTUMIA MADAWA HAYO KILWA KIVINJE

Hao vijana walioketi wanatumia madawa ya kulevywa wa Kilwa Kivinje lugha wanayozungumza ni ya ina yake .Mhariri  Msaidizi wa magazeti ya Kisomo vjijini Kanda ya Kusini Bw. Juma Nyumayo  mwenye suluali nyeusi anawahoji vijana hao,kwa nini wanatumia madawa hayo.wanadai kuwa hawana kazi ya kufanya,hivyo wakiyatumia madawa hayo wanakuwa bomba.
   Hivyo kwa hali hiyo tutawafikisha wapi vijana wetu ? ukweli ukiwaona vijana hao utawahurumia,wamekuwa kama mazezeta,tahira hivi.maana wanamawazo ya mbali sana,kwamba meli wana uwezo nazo katika kuzamia.

KILWA KISIWANI NA SONGOMNARA IMEWEKWA KWENYE URITHI WA DUNIA,BW.JUMA NYUMAYO MWANDISHI WA HABARI NA MHARIRI WA MAGAZETI YA KANDA TUJIFUNZE KUSINI ANASOMA KIVUKONI KWENDA KISIWANI

Bw.Juma Nyumayo aliyeshika kibao kilicho andikwa UNESCO- HIFADHI YA URITHI WA DUNIA,Kilwa Kisiwani na Songo Mnara,kibao kilichowekwa kabla ya kupanda maboti kwenda Kilwa Kisiwani ambako kuna majengo ya kihistoria na ustaarabu wa Kiarabu na Masultani na Ngome ya Wareno.
 Huyo ni mfanya kazi katika kivuko hicho ambaye kazi yake ni kutambulisha wageni/watalii wanaokwenda Kisiwani huko kuona mabaki ya majengo misikiti iliyojengwa enzi za biashara za waarabu zikiwemo za watumwa,pembe za ndovu.
UNESCO ndiyo wanaosaidia kufanya majengo yaliyoachwa yawe katika hali ya kuvutia na kupendeza .Tuna vivutio vingi pwani ya kusini mwa Tanzania.

Monday, May 28, 2012

Haya bado hayaja malizika kusombwa kwenye ghala la chakula la Taifa Ruhuwiko Songea ,na mengine yanavunwa sasa.kazi kwa walaji.

Shehena ya magunia ya mahindi ya zamani ambayo bado yanasombwa ,lakini pia wakulima wameanza kuvuna mahindi mapya katika Mkoa huo wa Ruvuma.Ni kazi kweli kwa walaji.

Hivi ndivyo ilivyo kuwa, Askofu wa Anglican Songea alivyo wahusia wakuu wapya wa wilaya baada ya kuapishwa

Bishop/Askofu wa Anglican aliwaambia ukweli wakuu hao wa Wilaya kuwa Mungu amewateua kwenda kuhudumia jamii,kwenda kutangaza amani na utulivu katika jamii wanayoikuta,kwenda kuongeza chachu ya maendeleo ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Ruvuma na mabungwa wa kuzalisha chakula kwa kilimo.
  Wananchi na Taifa linawategemea wao katika kuhamasisha wananchi kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.Hivi sasa wakuu hao wameunganika na wakuu wa mikoa,makatibu tawala wa mikoa kupata semina elekezi Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete

MWENGE WA UHURU MKOANI RUVUMA UTAFANYA KAZI YA KUKAGUA MIRADI 51 YENYE GHARAMA YA TSHS,1,930,357,902.



Gharama hiyo yenye mchanganuo wa uchangiaji wa gharama za miradi ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka  2012 ni kama ifuatavyo:-
  • Nguvu za wananchi Tshs.296,022,645/=
  • Halmashauri za wilaya na Manispaa Tshs.204,486,125/=
  • Serikali Kuu Tshs.773,599,581
  • Wadau wa Maendeleo Tshs.458,809,551/=
  • Watu Binafsi Tshs.287,440,000/=
Mwenge uko Mkoani Ruvuma Umepokelewa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma kutoka Mkoa wa Njombe katika Wilaya ya Nyasa na  kuanza kukimbizwa katika wilaya zote tano zenye Halmashauri sita ambazo ni Wilaya ya Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru.
    Ukiwa Mkoani Ruvuma Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kufungua miradi 13 yenye thamani ya Tshs.390,684,832 kuweka mawe ya msingi miradi 22 yenye thamani ya Tshs.1,303,187,695, kuzindua miradi 12 yenye thamani ya Tshs.141,045,375 na miradi 04 yenye thamani ya Tshs.34,840,000 itakaguliwa na kufanya jumla ya miradi yote kuwa 51 yenye thamani ya Tshs.1,930,357,902.
Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema “Sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau”.
Mwenge umekuwa ni kichocheo kikubwa cha shughuli za maendeleo, umoja, mshikamano na amani kwa Taifa letu.Lakini usemi wa Baba wa Taifa unaanza kuingia dosari Amani hiyo inaanza kutoweka,unasikia wenzetu Zanzibar Makanisa yanachomwa,tatizo hawataki Muungano sasa kukataa Mungano kuna uhusiano gani na Kuchoma makanisa ? Tunaelekea wapi sasa.



Sunday, May 27, 2012

Maisha in kuhangaika kila kukicha watu wnahangaika kutafuta ridhiki

 Kama hivyo foleni ya Malori yakisubiri kupakia mahindi ankuyapeleka Uganda,madereva wanakaa muda mrefu  hawaonani na familia zao yote hayo nikuhangaika kutafuata ridhiki.
Yote tisa huyo kijana anapgonga mawe katika Jiji la Mwanza ambako wameanzisha ujenzi wa barabara za mawe kutokana na uwingi wa mawe uliyopo katika Jiji hilo 'Rock City' anagonga mawe hayo kulingana na kipimo anachopewa anapata fedha za kwenda kumsaidia katika maisha yake.Maisha ni safari ndefu kila mmoja Mungu amempangia maisha yake,

RAIS KIWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAZAMANI 63 NA WAPYA 70 AMBAPO WAKONGWE MAJINA YAO HAYAPO



Tuna watakia uwajibikaji mwena wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu wakishirikiana na wadau wa sekta mbalimbali watakao wakuta katika wilaya walizopangiwa ,ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi.Mkoani Ruvuma Songea Joseph Joseph Mkirikiti,Tunduru Chande BaruUcho,Namtumbo Abdulah S.Lutavi,Mbinga Senvi S.Ngaga na Nyasa ( Mpya ) Ernest N Kahindi.Karibuni sana Ruvuma.

Majina na wilaya wanayokwenda wakuu wa wilaya za zamani 63 hayo:-

WAKUU WA WILAYA WA ZAMANI NA WILAYA WANAZOKWENDA  NI HAO

NA.    JINA           WILAYA ANAYO KWENDA
1.         James K. O. Millya             Longido
2.         Mathew S. Sedoyeka          Sumbawanga
3.         Fatuma L. Kimario             Igunga
4.         Capt. (Mst.) James C. Yamungu Serengeti
5.         Lt. (Mst.) Abdallah A. Kihato       Maswa
6.         Sarah Dumba          Njombe
7.         Jowika W. Kasunga            Monduli
8.         Elizabeth C. Mkwasa         Bahi
9.         Col. Issa E. Njiku    Misenyi
10.       John B. Henjewele Tarime
11.       Elias W. Lali            Ngorongoro
12.       Raymond H. Mushi            Ilala
13.       Francis Miti             Ulanga
14.       Evarista N. Kalalu             Mufindi
15.       Mariam S. Lugaila             Misungwi
16.       Anna J. Magowa     Urambo
17.       Anatory K. Choya   Mbulu
18.       Fatma Salum Ally Chamwino
19.       Deodatus L. Kinawiro        Chunya
20.       Ibrahim W. Marwa             Nyang’hwale (mpya)
21.       Dkt. Norman A. Sigalla     Mbeya
22.       Moshi M. Chang’a   Mkalama (mpya)
23.       Jordan M. Rugimbana       Kinondoni
24.       Georgina E. Bundala         Itilima (mpya)
25.       Halima M. Kihemba           Kibaha
26.       Manzie O. Mangochie        Geita
27.       Abdula S. Lutavi     Namtumbo
28.       Zipporah L. Pangani          Bukoba
29.       Dkt. Ibrahim H. Msengi    Moshi
30.       Col. Cosmas Kayombo       Kakonko (mpya)
31.       Lembris M. Kipuyo             Muleba
32.       Elinasi A. Pallangyo          Rombo
33.       Queen M. Mlozi       Singida
34.       Juma S. Madaha     Ludewa
35.       Angelina Mabula    Butiama (mpya)
36.       Hadija H. Nyembo Uvinza (mpya)
37.       Ernest N. Kahindi Nyasa (mpya)
38.       Peter T. Kiroya        Simanjiro
39.       John V. K. Mongella           Arusha
40.       Baraka M. Konisaga          Nyamagana
41.       Husna Mwilima       Mbogwe (mpya)
42.       Sophia E. Mjema     Temeke
43.       Francis Isaac           Chemba (mpya)
44.       Abihudi M. Saideya            Momba (mpya)
45.       Khalid J. Mandia    Babati
46.       Anna Rose Nyamubi          Shinyanga
47.       Dani B. Makanga    Kasulu
48.       Amina J. Masenza Ilemela
49.       Mercy E. Silla          Mkuranga
50.       Christopher R. Kangoye    Mpwapwa
51.       Lt. Edward O. Lenga          Kalambo (mpya)
52.       Halima O. Dendego            Tanga
53.       Lephy B. Gembe      Dodoma
54.       Saidi A. Amanzi      Morogoro
55.       Jackson W. Msome             Musoma
56.       Elias C. B. Goroi      Rorya
57.       Lt. Col. Benedict Kitenga Kyerwa (mpya)
58.       Erasto Sima             Bariadi
59.       Nurdin H. Babu      Mafia
60.       Khanifa M. Karamagi        Gairo (mpya)
61.       Gishuli M. Charles             Buhigwe (mpya)
62.       Saveli M. Maketta Kaliua (mpya)
63.       Darry Rwegasira     Karagwe

MAJINA 70 NA WILAYA WANAZOKWENDA WAKUU WA WILAYA HAO WAPYA NI HAO:-

1.         Novatus Makunga Hai
2.         Mboni M. Mgaza     Mkinga
3.         Hanifa M. Selungu             Sikonge
4.         Christine S. Mndeme         Hanang
5.         Shaibu I. Ndemanga          Mwanga
6.         Chrispin T. Meela   Rungwe
7.         Dr. Nasoro Ali Hamidi       Lindi
8.         Farida S. Mgomi     Masasi
9.         Jeremba D. Munasa           Arumeru
10.       Majid Hemed Mwanga      Lushoto
11        Mrisho Gambo         Korogwe
12.       Elias C. J. Tarimo   Kilosa
13.       Alfred E. Msovella Kiteto
14.       Dkt. Leticia M. Warioba    Iringa
15.       Dkt. Michael Yunia Kadeghe       Mbozi
16.       Mrs. Karen Yunus Sengerema
17.       Hassan E. Masala   Kilombero
18.       Bituni A. Msangi    Nzega
19.       Ephraem Mfingi Mmbaga            Liwale
20.       Antony J. Mtaka     Mvomero
21.       Herman Clement Kapufi   Same
22.       Magareth Esther Malenga           Kyela
23.       Chande Bakari Nalicho     Tunduru
24.       Fatuma H. Toufiq   Manyoni
25.       Seleman Liwowa     Kilindi
26.       Josephine R. Matiro           Makete
27.       Gerald J. Guninita Kilolo
28.       Senyi S. Ngaga        Mbinga
29.       Mary Tesha Ukerewe
30.       Rodrick Mpogolo     Chato
31.       Christopher Magala           Newala
32.       Paza T. Mwamlima            Mpanda
33.       Richard Mbeho        Biharamulo
34.       Jacqueline Liana    Magu
35.       Joshua Mirumbe     Bunda
36.       Constantine J. Kanyasu    Ngara
37.       Yahya E. Nawanda            Iramba
38.       Ulega H. Abadallah            Kilwa
39.       Paul Mzindakaya   Busega (mpya)
40.       Festo Kiswaga         Nanyumbu
41.       Wilman Kapenjama Ndile            Mtwara
42.       Joseph Joseph Mkirikiti    Songea
43.       Ponsiano Nyami      Tandahimba
44.       Elibariki Immanuel Kingu           Kisarawe
45.       Suleiman O. Kumchaya    Tabora
46.       Dkt. Charles O. F. Mlingwa          Siha
47.       Manju Msambya     Ikungi (mpya)
48.       Omar S. Kwaangw’             Kondoa
49.       Venance M. Mwamoto       Kibondo
50.       Benson Mpesya       Kahama
51.       Daudi Felix Ntibenda        Karatu
52.       Ramadhani A. Maneno     Kigoma
53.       Sauda S. Mtondoo   Rufiji
54.       Gulamhusein Kifu Mbarali
55.       Esterina Kilasi        Wanging’ombe (mpya)
56.       Subira Mgalu           Muheza
57.       Martha Umbula      Kongwa
58.       Rosemary Kirigini Meatu
59.       Agness Hokororo     Ruangwa
60.       Regina Chonjo         Nachingwea
61.       Ahmed R. Kipozi     Bagamoyo
62.       Wilson Elisha Nkhambaku          Kishapu
63.       Amani K. Mwenegoha       Bukombe
64.       Hafsa M. Mtasiwa   Pangani
65.       Rosemary Staki Senyamule         Ileje
66.       Selemani Mzee Selemani Kwimba
67.       Lt. Col. Ngemela E. Lubinga       Mlele (mpya)
68.       Iddi Kimanta           Nkasi
69.       Muhingo Rweyemamu      Handeni
70.       Lucy Mayenga         Uyui



MAUAJI YA WASICHANA KATIKA MANISPAA YA SONGEA YANAANZA KUREJEA TENA BAADA YA UTULIVU ULIYO PATIKANA BAADA YA MACHAFUKO YALIYOTOKEA KATIKA MJI WA SONGEA.

Msichana wa ambaye jina lake halikutambulika kupitia blog hii mkazi wa Mombambili ambaye alikuwa mamantilie amekutwa amekufa Jirani na Kambi ya JWTZ Ruhuwiko inasemekana kifo chake kilihusishwa na mambo ya kimapenzi.Inaelekea alichukuliwa na Mvulana toka Mombambili hadi Ruhuwiko Manispaa ya Songea,kisha kufanyiwa vitendo vibaya na kuuwawa na kutupwa kwenye mpenyo wa nyumba inayotarajiwa kuwa nyumba ya kulala wageni Polisi wanaendelea na uchunguzi uliyosababisha kifo hicho.
Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma ulikuwa shwari na kurejesha amani,sasa wimbi la mauaji linataka kurudia tena,sijui tatizo liko wapi,watu kuua watu wenzao hawaoni shaka,wala mwili kusisimka,amakweli shetani ananguvu,ni muhimu kukemea matukio hayo maovu,

JUMAPILI YA SIKUKUU YA PENTEKOSTE ,MITUME WALISHUSHIWA ROHO MTAKATIFU

Ilipofikiam siku hamsini baada cha kifo chake Yesu Kristo,aliwatokea mitume wake waliyojifungia ndani kwa kukata tamaa,kwani waliyemtegemea aliuawa.
Basi walishushiwa Roho Mtakatifu kwa ishara ya ndimi za moto,nakuwaambia kuwa mtakao waondolea dhambi wataondolewa na mtakao wafungia dhambi watafungiwa.Roho mtakatifu inatia nguvu,inaleta amani,nyumba isiyo na Roho mtakati haina amani,Ofisi isiyo na Roho mtakatifu haina mshikamano wa kuleta maelewano ndani ya kazi,
Ukosefu wa Roho Mtakatifu Katika Mataifa ndiyo sababu ya mahangaiko ya maisha,amani hakuna,uaminifu uanapungua,chuki,dharau,unyanyasaji,dhuluma ukiukwaji wa haki za binadamu unatawala katika mataifa mengi,Serikali ni watu ,na watu hao wakikosaka nguvu ya Roho Mtakatifu wananchi wake watahangaika,kwa manung'uniko ya hapa na pale kwa kukosa mahitaji yao muhimu ambayo walitegemea serikali yao iwatekelezee.Hivyo Jumapili ya leo ni ya Muhimu sana kwetu binadamu.Nawatakia Jumapili inayomalizika njema.'Amani na iwe kwenu' Aliwaambia Mitume wake ambo walikosa Amani.

Thursday, May 24, 2012

EASY TECH. COMPUTER TRAINIG CENTRE SONGEA - RUVUMA TANZANIA ' NDIYO JIBU KWA MATUMIZI YA MITANDAO YA INTERNET'

Mkurugenzi wa Easy Tech Bw.Peter Mpelesoka anasema kuwa hakuna jibu zaidi la mtu kutumia mitandao ya Internet bila kupitia katika mafunzo ya awali ya computer,Alisema kuwa chuo hicho kinachukua wanafunzi wa vyuo mbalimbali ambao walikuwa hawana knowledge ya computer aidha wafanyakazi katika ofisi ambazo hazina ama zina computer alipenda kuzitumia.
Alisema pamoja na kujifunza Programme mbalimbali lakini pia wanajifunza na matumizi ya Internet jambo ambalo katika kipindi hiki cha Sayansi na Teknolojia ni vyema watu waelewe matumizi ya mitandao hiyo maana Dunia imekuwa kama kijiji.Chuo kipo Ok Hotel mkabala na Bekari ya mikate ,ukiingia Mjini Songea Uliza Easy Tech Computer Training Centre  watakuelekeza.

EASY TECH. COMPUTER TRAINIBG CENTRE SONGEA - RUVUMA TANZANIA ' NI UKOMBOZI WA VINA NA WATU WAZIMA WA KUJIFUNZA COPYUTA'

 Darasa la wanafunzi wanaojifunza Computer katika Chuo hicho cha 'Easy Tech.Computer Training Centre.Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mwalimu  Ally Mamis akiwaelekeza wanafunzi wake waliyoingia mchana leo.

Wanafunzi wa Programme mbalimbali wakiwa makini katika kujifunza kwa vitendo.


Mkurugenzi wa Chuo hicho Bwana Peter Mpelesoka akiwa kwenye shughuli za' Designing' anasema ni zaidi ya wanafunzi 2,000 wamepitia katika chuo chake ambao wamefaidika mafunzo ya Computer katika hatua tofauti.

Tuesday, May 22, 2012

machungwa ya kisasa ya muda mfupi yanapatikana chuo kikuu cha kilimo SUA Morogoro

 Chuo Kikuu cha Kilimo SUA Mororgoro kina miche ya matunda ya kila aina ambayo inazaa kwa muda mfupi, kama michungwa,mipare,migomba mastafeli na minazi.
Ni chungwa ambao hata mtoto mdogo anaweza kuchuma,huu ni mchungwa niliyoupata SUA pamoja na mstafeli ambao na wenyewe unazaa.nyumbani Morogoro.

Saturday, May 19, 2012

SPACIAL OFFER FOR AURIC AIRLINES - SONGEA -DAR ES SALAAM - DAR ES SALAAM TO SONGEA

 Fare for Foreigners is 472,000/= for one way,and Citizen is 325,000/= one way or if a Citizen can pay before one week is 250,000/= one way.
For booking contact Abbas Stationery as an Agent Mob.0713 - 645966 SONGEA RUVUMA- TANZANIA  Timetable of the journey is as for days per week as  follows:-
  • Monday
  • Tuesday
  • Thursday and
  • Friday  
Fly with Auric Airlines Songea to Dar and Dar to Songea to minimize time spend by bus with tank.

Thursday, May 17, 2012

MAONI NA USHAURI WA VIONGOZI WA DINI WA WADAU WENGINE USIKU

Mwasisi na mkuu wa mikoa zamani Mzee Songambele awapa maneno ya kujenga wakuu hao wapya katika Mkoa huo.Zaidi wengine Usiku nawatakieni ushirikiano mwema katika kutumia mtandao huu wa Blog.

MWAMBUNGU AWAMBIA WAKUU WA WILAYA KUFANYA KAZI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI,WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA WANATEGEMEA KILIMO KWA MAISHA YAO,SASA DHAMANA KUBWA WAMEPEWA KUONGEZA MAENDELEO ZAIDI

 Mwambungu 'asema mmekabidhiwa dhamana kwenye wilaya zenu,wananchi wanategemea sana ushirikiano wenu katika kuendeleza maendeleo,Mkoa huu unategemea sana kilimo,hivyo wananchi wanategemea pembejeo za kilimo ,isitoshe mkoa una vyanzo vingi vya uchumi vyote vitategemea dhamana mliyopewa'
Aidha alisema kuwa mkoa huo uko nyuma katika elimu,hivyo dhamana waliyo pewa watajitahidi kuwa kushirikiana na sekta ya elimu na wananchi katika kuinua taaluma, alisema wafanye kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na kutekeleza kanuni za Ilani ya Chama  ( CCM ).Leo ameapisha wakuu wa wilaya watano ambao ni wa Wilaya ya Nyasana Ernest N Kahindi,Namtumbo Abdula Suileman,Songea Joseph Joseph Mkirikiti,Mbinga Senyi Simon Ngaga na Tunduru Chande Bakari Nalicho.
Picha ya pamoja na viongozi Mbalimbali Mkoani
 Picha ya pamoja na mataji wakuu hao wa wilaya na Mkuu wa mkaoa
Picha ya pamoja ya ukumbusho wao bila mataji.Kati yao Mama mmoja , wananchi wa mkoa wa Ruvuma wanawategemea sana katika kilimo,kupata soko bila ubabaishaji.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID THABIT MWAMBUNGU AAPISHA WAKUU WAWILAYA WATANO ( 5 ) LEO AKIANZA NA MKUU WA WILAYA YA NYASA

 Mkuu wa Wilaya mpya ya Nyasa  Ernest N Kahindi alianza kuapa
 Akafuatiwa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Abdul Suliman Lutavi
 Akaja Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph josehp Mkirikiti
 Baadaye akaapa mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Simon Ngaga
Hatimaye mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Bakari Nalicho ,akafunga dimba.wakuu hao baada ya kuapa na kusaini walikabidhiwa vifaa vya kufanyika kazi na Mkuu wa mkoa mhe.Said Thabit Mwambungu,walipewa katiba ya nchi na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ndiyo imewapeleka pale walipo leo

Wameapa na kuahidi kuwa watakuwa waaminifu na kutekeleza kanuni za katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Sunday, May 13, 2012

HONGEARA REO RUVUMA KUWA MKURUGENZI WA SEKONDARI,BIBI PAULINA MKONONGO MATUNDA YA KAZI YAKE YAMEJIONYESHA ,AENDELEE HIVYO KATIKA NAFASI HIYO

 Afisaelimu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa sekondari.Bibi Mkonongo anastahili kabisa kupata nafasi hiyo kutokana na kazi zake za ufuatiaji wa taaluma katika mkoa huo.Anauchungu na jamii inayohitaji kuelimishwa kwa uhakika,pamoja na changamoto nyingi zilizopo kwenye Sekta ya elimu.Tunamtakia kazi njema huko aendako.
Bibi Mkonongo wa kwanza kulia akimtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul Mushi watatu kushoto na wa katikati ni kaimu RAS Mkoani Ruvuma Injinia Tossi,kwa wadau wa elimu katika ukumbi wa maliasili mkoa Mjini Songea hivi karibuni.Kwenye kikao cha kazi kuhusu mitaala ya elimu.

Ambapo Dkt Mushi alifafanua kiundani kuhusu imani potofu ya baadhi ya wananchi kulaumu kuwa elimu inashuka kutokana na mabadiliko ya mitaala ya elimu kila kukicha.Alisema si kweli bali kuna maboresho ya mitaala hiyo.

Saturday, May 12, 2012

SIKU YA WAUGUZI DUNIANI,KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA SONGEA WAUGUZI WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZINAZO FANYA WASHINDWE KUTIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO.

 Maandamano ya wauguzi wa hospitali ya mkoa ya Songea wakielekea kwenye viwanja vya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo watapata nasaha kutoka kwa mgeni rasmi wa siku ya muuguzi duniani.
Wauguzi hao wanakabiliwa na changamoto kadhaa zinazofanya wasitekeleze kazi yao ngumu kama inavyo takiwa,lakini kutokana na changamoto hizo wauguzi hao bado wanafanya kazi yao kadri wanavyo weza za kuhudumia wagonjwa.
Muuguzi Mama Mbano alisema kuwa changamoto kubwa zinazowakabili ni pamoja na .Ukosefu wa vitendea kazi na kama vipo havitoshelezi kulingana na idadi ya wagonjwa wanavyo fika kutibiwa katika hospitali hiyo.Nyingine ni upungufu wa madawa,hazitoshelezi mahitaji ya wagonjwa ikizingatiwa Songea hospitali ni hospitali ya Mkoa. pia na upungufu wa wauguzi ,hawatoshelezi  ukilinganisha na ukubwa wa hospitali hiyo.

Friday, May 11, 2012

Polisi Jamii Kata ya Mshangano imepunguza kwa kiasi kikubwa vitendo viovu walivyokuwa wakifanya vijana kata hiyo.


 Kamanda mkuu wa usalama kata ya Mshangano Bwana Wolfugang,anasema kuwa kuna vikundi viwili vya ulinzi shirikishi cha kwanza ni cha ulunzi jamii na cha pili ni cha sungusungu ambavyo vinalinda usiku na mchana.anasema tandu zoezi hilo la ulinzi lianze vitendo vya wizi wa mifugo,uvutaji wa bangi kwa vijana vimepungua sana.
 Kikundi cha Lizombe kilitumbuiza katika hafla fupi ya kurekodi kipindi cha ulinzi shirikishi,Polisi Jamii Kata ya Mshangano leo.
 Inspector Paul Mashimbo anasema kazi ya polisi ni kutoa taaluma kwa wananchi maana kazi ya ulinzi ni jukumu la kila mmoja kuwa mlinzi katika sehemu yake,maana ulinzi na usalama siyo kazi ya askari polisi peke yao. alisema hayo katika mahojiano na Channel Ten Mshangano Manispaa ya Songea leo.
 Inspector Paul Mashimbo akisalimiana na viongozi wa Kata ya Mshangano wakiwemo Watendaji wa kata za Mshangano,Msamala,na Shule ya Tanga.
RTO  wa usalama Barabarani ambaye ni mlezi wa Ulinzi na usalama Kata ya Mshangano,anasema kuwa ulinzi ni jukumu la kila mwananchi wakishirikiana na Polisi kata ili kudhubiti uhalifu unaotokana na jamii kuvunja maadili.pomoja na usalama wa raia na mali zao.

JENGO LA DAWATI LA POLISI WANAWAKE KITUO CHA POLISI SONGEA MJINI,LITASAIDIA KUTOA ELIMU KWA JAMII INAYOKUBWA NA MATATIZO YA KIBINADAMU

 Jengo la Dawati la mtandao wa polisi wanawake Songea Mjini kwa mbele hadi
 Jango hilo kwa nyuma
 Kaimu  Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma George Chiposi wa kwanza kushoto.
 A/Insp.Fadhilia Marwa Chacha anasema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia sana kupunguza unyanyaswaji wa wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa kwa kupata mafunzo kupitia mtandao huo.
Inspector wa Polisi na mwenyekiti wa ujenzi wa jengo hilo ,pia ni mkuu wa upelelezi wa Wilaya ya Songea Anna Tembo anasema jengo hilo mpaka kufikia hatua hiyo limeshaghalimu Tshs.milioni 10 laki tano.