Wednesday, February 1, 2012

MGOMO WA MADAKTARI UKICHANGIWA NA POSHO KUBWA YA WABUNGE UNAWAPASUA WATU VICHWA

 Waandishi wa habari Bwana Juma Nyumayo kushoto mwenye shati na Benson Mapundwa kulia mwenye T - Shirt yenye ufito mwekundu wakijadiliana jinsi Serikali ilivyo amua kuhusu mgomo wa madaltari ,ambao Mhe.Waziri mkuu Mizengo Pinda alivyo waambia madaktari hao kufanya ili kuinusuru ajira yao.
Aidha mkanganyiko unajitokeza pale wabunge walipojipangia posho ya shilingi 200,000 kwa siku,hilo bado wananchi wengi wanashindwa kuelewa,na maswali maengi wanajiuliza,kama serikali inauwezo wa kuwalipa wabunge posho ya shilingi 200,000 kwa kikao,kwanini watumishi wa Umma wakiwemo Madaktari hao wasilipwe wanacho dai?.
Tufike mahali tutambue kila mtumishi ana umuhimu wake pale alipoajiriwa,na anastahili kulipwa kulingana na mabadiliko ya maisha hasa kwenye mfumuko wa bei.
Kinacho leta shida ni pale wanaogoma wanapokosa mshikamano wa kupanaga wagome vipi,na wakigoma je serikali ina fedha za kuweza kulipa wanacho kidai.
Ndiyo maana serikali imechukua uamuzi mgumu wa kuwapa masharti madaktari kurejea kazini ama kuendelea na mgomo,ili serikali ifanye juhudi za kutafuta madaktari wengine kwa lengo la nusuru maisha ya watanzania wasio na hatia.Kweli leo Madaktari kutoka jeshini wako Muhimbili wanafanya kazi,Ingwa sijambo zuri kuwanyima madaktari hao wanacho kidai,lakini pia si vibaya serikali kuwaweka pembeni hadi hapo itakapo kuwa na uwezo wa kuwatekelezea wanacho kidai.wakati maisha ya wananchi ipo kwenye usalama.

No comments:

Post a Comment