Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal apokewa viwanja vya Ikuli ndogo Songea.
Kikundi cha Lizombe cha zawadiwa bahasha na mama Asha Bilal katika viwanja vya Halmashuri ya Manispaa ya Songea
Makamu ahutubia baadhi ya viongozi wa chama na serikali na wananchi wakiyofika kumpokea Ikulu ndogo Songea
Mkurugenzi matendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea akimkabidhi taarifa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu.
Kikundi cha lizombe toka Lizaboni Manispaa ya Songea kikitumbuiza
Mama Asha Bilal akiwasalimia wananchi na kuwapongeza kwa juhudi kubwa wanazozionyesha kwenye Sekta ya kilimo.
Makamu wa Rais akielezea jinsi serikali inavyo thamini mchango wa wananchi katika kilimo na jinsi inavyoruhusu watu wenye fedha zao wanunue mahindi kwa bei ya shilingi 350 kwa kilo na wao wayauzi kokote ndani na nje ya nchi.wakati akiwa kwenye ghala la hifadhi ya chakula la taifa Ruhuwiko.
Hayo ni mahindi ambayo yamehifadhiwa nje ,baada ya maghala kujaa mahindi,ambayo sasa yanachukuliwa na kusafirishwa.

MAKAMU wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal alikuwa na ziara ya
kikazi katika mkoa wa Ruvuma ambako
alikagua,kutembelea miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa Uranium Wilayani
Namtumbo,Ghala la taifa la kuhifadhi chakula Ruhuwiko Songea na Makaa ya mawe
Rwanda Mbinga.
Ziara ya makamu wa
Rais imefanyika kwa mafasniko makubwa ingawa sintofahamu zilijitokeza kwenye
mrdi wa Uranium,Makamu hakufikishwa kwenye mgodi ili akague eneo la mradi kama ilivyo onyeshwa kwenye ratiba ya matukio ya ziara
hiyo.
Watu wanajiuliza kwanini Dkt hakufikishwa kwenye mradi huo
mkubwa amabo bado kuanza kuzalisha,Kama hiyo haitoshi kwanini Wizara ya Nishati
na madini isipaleke mwakilishi wake au mataalamu wake, kama
waziri wa nishati alikuwa na udhuru?.
Kumbe watu wa chini kabisa ambao hawasikilizwi wasemayo ,kumbe
walalamikayo ni sahihi,kuwa kila siku kuna helkopta zinatua huko na kuondoka na
madini,na kwamba maeneo mengi huko ni mashimo matupu je zinachimbwa Uranium
peke yake au kuna madini mengine ambayo yanaibiwa bila ya kueleweka ? kama ni uongo sasa kwa nini makamu wa Rais hakupelekwe
kwenye eneo la mgodi ili ajionee mwenyewe.
Wa- Tanzania tutaibia maliasili zetu mpaka lini na hao
wanaoitwa wawekezaji kutoka nje? Lakini hatuwezi kushangaa kama
twiga kwenye hifadhi ya taifa waliweza kupitishwa na kusafirishwa nje ya nchi
kwenye ndege sembuse,madini ambayo yako mbali na mkoa na wilaya.
Hapo kuna mchezo mchafu unafanyika, na hao waliyowekeza
kwenye mradi huo na baadhi ya watendaji katika wizara hiyo,huwenda na wadau
wengine,kwa utaratibu huo nani amfunge paka kengele ? ( ama kweli mikataba ya
madini itatumaliza ).
Sera ya madini Tanzania ni wizi mtupu. Serikali yenyewe imekuwa ikituambia kuwa inaipitia upya mikataba mibovu ya madini, ili kuzuia hasara inayolipata Taifa, na ili Taifa liweze kufaidika na madini hayo.
ReplyDeleteSasa suali langu ni je, hao waliosaini hiyo mikataba mibovu walikuwa wajinga wasioelewa kilichoandikwa, au walikuwa wamelewa gongo, au walikuwa ni mafisadi tu? Na je, ni akina nani hao, na kwa nini hawajawajibishwa?
Hiyo ni hoja ninayojenga kutokana na kauli ya serikali yenyewe kuhusu kuwepo kwa mikataba mibovu.
Zaidi ya hapo, nami nasikia sana kuwa ndege zinatua na kuondoka kwenye hiyo migodi, na hatuelezwi wazi kinachoendelea. Wiki chache zilizopita, kule Nzega, majambazi walitaka kuitungua ndege iliyokuwa ikiondoka na shehena ya dhahabu. Na ndege hizo zinaondoka mara kwa mara kwenye migodi mbali mbali.
Papo hapo, wakati nchi yetu ina utajiri mkubwa wa madini, bado ni nchi mojawapo inayoongoza kwa kutegemea hiyo inayoitwa misaada kutoka nchi zingine. Ni ujinga mkubwa sana kwa nchi yenye rasilimali kama Tanzania kuwa katika kundi la nchi zinazotegemea hiyo inayoitwa misaada.
Dhahabu yetu inawatajirisha wanahisa wa kampuni kama ya Barrick Gold. Ila Tanzania kwenyewe tunapigwa changa la macho na hayo makampuni, kwa kushirikiana na serikali yetu wenyewe.