MTAALAMU
huyo alisema kuwa enzi hizo za utawala wa kigeni Zanzibar
ulikerwa na uchafu katika mji Mkongwe,hivyo waliamua kuwambia watawala wenzao
walioko India
wawaletee kunguru hao ili wasaidie kupunguza uchafu.
Kutoka
miaka hiyo kunguru hao wakawa wengi Zanzibar,wakiwa
wakisaidia kuondoa uchafu siyo mji Mkongwe peke yake bali Zanzibar yote,Kunguru hao wamekuwa
kero,wanasababisha kuchafua mazingira kutokana na kula kila kitu wanacho kiona.na
kukiacha hapo na kuondoka zake.
Isitoshe
kunguru hao sasa wamekuwa kero pia katika Jiji la Dar es Salaam,Mhimbili,Osheni
Road,Temeke,Fery na maeneo yote yenye
dalili ya vyakula.Kunguru wale sio waoga kamwe wako tayari kuchukua nyama au
samaki zilizoanikwa mbele ya mwenye samaki au nyama yake.
Aidha
kunguru hao wanauwezo mkubwa wa kusambaza vimelea vya maradhi,kwakuwa wanaweza
kutoka kula mzoga, na hatimaye wakatua kwenye vyakula vya watu na kuacha
vimelea vya maradhi kwenye chakula kile. Je habari hizo ni za kweli? Kwamba kunguru
hao walichukuliwa India
? waliletwa kanguru au mayai yao,
na kweli wanakera ?
Kuhusu
kunguru je wale wenye baka jeupe wao hawasumbui isipokuwa kunguru weusi pekee ?
Mwaka Fulani nilikuwa Ward ya Mwaisela Muhimbili Jijini Dar es Salaam,kwenye
corridor kunguru mwenye baka jeupe alikwapua vipande vya mikate ya wagonjwa
kwenye kigari alichokuwa akikisukuma muuguzi mbele yake alipotaka kuingiza
ndani .
Kama
kweli wanakera na wanaleta madhara kwa afya ya binadamu,sasa kifanyike nini
kuwapunguza kunguru wote weusi na wenye baka jeupe,kwani kunguru wamezagaa Tanzania nzima
hasa wale wenye baka jeupe.
No comments:
Post a Comment