Tuesday, February 14, 2012

DOKTA MOHAMED GHARIB BILAL AMALIZA ZIARA YAKE SIKU YA KWANZA KWA KUZUNGUMZA NA WANANCHI NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UKUMBI WA MIKUTANO MANISPAA YA SONGEA

 Anakata utepe kwenye jiwe la msingi la ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Songea ,ukumbi huo ukimalizika utakuwa umegharimu shilingi 285,800,000.
 akiongea na wananchi ambao wamepewa pongezi kwa uzalishaji wa chakula na ziada ya kuuza nje ya mkoa,Aidha alisema serikali itahakikisha mahindi yote yatanunuliwa,ili wanaonunua mahindi hayo kwa mkulima kwa bei ndogo wakose mwanya huo.
 Ziara hiyoa ilijumuisha wabunge wa majimbo yote ya Mkoa wa Ruvuma ,ambapo Mbunge wa Songea Mjini Mhe.Emannuel Nchimbi alipata nafasi ya kuongea na wapiga kura wake.
 Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama akipeana mkono na Makamu wa Rai Dkt Bilal.
 Shaghuli zote za ziara ili zitambulike lazima waandishi wa habari lazima wawepo,Waliokaa hapo ni baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma,pia ni wanachama wa Ruvuma Press Club,ingawa kuna baadhi ya wadau wa habari hawatambui kuwepo kwao,ila wanapenda watambulike,sijui utatambulika vipi ikiwa huwatambui ?
 Dkt Bilal atia saini kitabu cha wageni alipowasili viwanja vya bustani ya Halmashauri walipomwandalia kwa shughuli za ziara hiyo.
 Alipokelewa na kikundi cha Lizombe ngoma maarufu mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Thabit Mwambungu akimaribisha Mhe.Makamu wa Rais Meza ya kukaa iliyo andaliwa kwa ajili yake.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bwana Mwambungu akisalimia wananchi ili atambulishe msafara wa Makamu wa Rais ambapo,tarehe 15/2/2012 atafanya ziara yake Wilaya ya Namtumbo kisha kukagua mradi mkubwa wa URENIUM.na kurudi Songea.

1 comment:

  1. Shukrani kwa taarifa hizi. Unafanya kazi nzuri sana ya kutuhabarisha hata sisi tulioko ughaibuni. Nimepangia kuja Songea mwezi ujao. Ninategemea itawezekana kukutana na wana Ruvuma Press Club, kama mwaka jana. Na labda tutaweza kuongea kwa undani zaidi na kutafuta namna ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya jamii yetu.

    ReplyDelete