Monday, February 6, 2012

WATANZANIA JANA WALISHEHEREKEA MIAKA 35 YA KUZALIWA KWA CCM,MWEZI REBRUARI TAREHE 5 1977 LAKINI UMEKUWA MWEZI MGUMU KIMAISHA

TAREHE 5 Februari 1977 Chama Kipya kilizaliwa,Naikumbuka siku na mwaka huo,kwenye shule za msingi nchini waliimba kwa mtindo huu.'kuzaliwa kwa Chama kipya,tahere 5 mwezi wa pili  sabuni na saba ewe Mungu kipe baraka'.kipindi hucho kulikuwa na nidhamu shuleni ,wanafunzi walijua nini wanachotakiwa kufanya,na kwanini wapo shuleni.napia waliheshimu walimu wao wanao wafundisha.

Aidha kwa upande wa walimu nao waliwajibika,walijituma katika kufundisha,ingawa maslahi yalikuwa madogo kulingana na wakati huo,lakini walijitoa kuhakikisha wanafunzi wanaelewa na wanafanya vizuri katika mitihani yao,isitoshe ratiba ya masomo iliheshimiwa ikiwa ni pamoja na mitaala,siyo kila kukicha inabadilika,lakini mwalimu hapelekwi kwenye mafunzo ya mtaala mpya.

Hayo tisa, hijyo jana siku ya kusheherekea siku hiyo,baadhi ya wananchi hasa wafanya kazi wananung'unika kuwa hali ya fedha ni mbaya,wanasema ni mwezi mgumu sana kimaisha.mabuchani nyama hazimaliziki,samaki kwenye majokofu hali ni mbaya,na ukijumuisha na hali ya umeme ilivyo ya manati katika Manispaa ya Songea,basi hakuna tofauti na waliyoishi karne ya ujima.Hiyo ndiyo Songea imo ndani ya Mkoa wa Ruvuma grid ya taifa ni ndoto katika mkoa huo,lakini wote tulisheherekea kuzaliwa kwa CCM.ndani ya giza totolo.

No comments:

Post a Comment