Wednesday, February 22, 2012

MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATOA RAI YA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO NA UONGOZI WA MKOA PANAPOTOKE VITENDO VYA UHALIFU

 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bwana Said Thabit Mwambungu aongea na wandishi wa habari ofisni kwake leo kupitia vyombo vya habari,kuwaomba wananchi kuwa na uvumilivu wakati serikali ,inafanya jitihada za kutafuta vyanzo vya matukio ya mauaji yaliyotokea siku tatu mfululizo katika Manispaa ya Songea.
Aidha ameomba ushirikiano wa uongozi wa mkoa na viongozi wa mitaa,kata na tarafa wa kuwa na ulinzi shirikishi,kwa kuwa wahalifu wanaishi nao.

Aidha alisema vifo vingi vinasadikiwa vinatokana na imani za ushirikina na uchawi basi na majambazi waningilia hapohapo katika mauaji ya watu,hivyo matembezi ya usiku kama sio ya lazima yaachwe kupisha polisi na ulinzi shirikishi ufanye kazi yake.Na kwamba indapo mtu asiyejulikana,mara moja itolewe taarifa mapema kabla uhalifu haujatokea.
z
 Waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa mkoa,alipokuwa akiwataka wananchi wasubiri serikali ifanye kazi yake kushirikiana na viongozi wa mkoa na wananchi kuhakikisha hali ya utulivu inakuwa kama awali,kufuatia maandamano ya wananchi yaliyozuiwa na polisi kwa kutumia mabomu na silaha za moto kuzuia,ambapo watu wawili wamepoteza uhai wao kutokana na majibishano ya mabomu na mawe yaliyokuwa yanatupwa na wananchi.katika manispaa ya Songea leo.
Ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma akiwa na waandishi wa habari

1 comment:

  1. Niko huku ughaibuni, na leo nimepiga simu Songea. Ninahisi kuwa kuhusu haya yaliyotokea Songea, inabidi tupate maoni na mitazamo yote iliyopia. Pamoja na kutuletea mtazamo wa serikali, waandishi wa habari watuletee mtazamo wa wananchi, wakiwemo waendesha piki piki. Katika mchakato huu mpana bila shaka tutajua chanzo cha tukio hili la kusikitisha, na mikakati ya kutatua, ili Songea iendelee kuwa na amani kama zamani.

    ReplyDelete