WATU
sita ( 6 ) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa ujambazi wa kutumia
milipuko,mapanga na visu,Mkongotema Tarafa ya Madaba Mkoani Ruvuma usiku wa
kuamkia tarehe moja Februari mwaka huu.
Kamannda
wa Polisi wa mkoa huo,Kamanda Michael Kamuhanda amewambia wandishi wa habari
kuwa majambazi hao kabla ya kufanya uhalifu huo walipofika kwa Bwana Remigius
Ngunja walipiga milipoko mine hewani kutishia wanakijiji wasiweze kutoa msaada.
Kamanda
Kamuhanda aliyataja majambazi yahu kuwa ni pamoja na Baraka Beda ( 25 ) mkazi
wa Morogoro,Salum Ahmadi ( 45 ) mkazi wa Mtwara na Stanley Mtega ( 20 ) mkazi
wa Ludewa.
Na
wengine walikamatwa kwenye msko wa polisi ni pamoja na Peter Mbilinyi ( 25 )
,mkazi wa Mkongotema,Mfalme Rashidi ( 30 ) mkazi wa Hanga Ngadinda na
Jemsi Mtewele ( 21 ) mkazi wa magingo.
Alisema
wote kwa pamoja wako mahabusu wakati upelelezi ukiendelea,kwa tuhuma za kukutwa
na milipuko ,ambayo hutolewa kwa kibali
kwa wachimba madini,barabara ,na vikosi vya usalama.
Alisema
majambazi hayo yalikwenda nyumbani kwa Bwana Remigius Nguja na kuwamuru atoe
fedha,aliposita basi walimkatakata kwa mapanga kichwani,mgongoni na
mikononi,kisha wakamwendea mkewe Bibi Oktaviana Danda wakamtishia kuwa watamkata mikono ndipo
walipowapa zaidi ya shilingi 3,000,000 na kutokomea gizani.
Baada
ya bkufanya uhalifu hu walikwenda kwa nyumbani kwa Bwana Igno ambapo walimkuta mlinzi Bwana Awito
Mbilinyi,kwa kuona hivyo aliwaonyesha kwa boss kwa kuwa hawamjui naye
aliwaambia Boss hayupo labda mkamuulize mke wake.ataambia alipo.
wakamuuliza boss wako yuko wapi,
Kamuhanda
alisema majambazi hayo yalikuwa yakifuatilia fedha shilingi 15 milioni ambazo
walisikia mtu mmoja katika kijiji hicho anazo bila ya kuwa na uhakika na mwenye
fedha.
Walipomwendea mke wa Igno kumuuliza Igno
alipata mwanya wa kutoroka majambazi ,Mkewe alibakia na kizazaa cha kuonyesha
fedha zilipo, na kuporwa shilingi 1,026,000.
Aidha
Kamuhanda alisema baada ya msako wa polisi wa Madaba wakishirikiana na Polisi
wa Songea Mjini , waliwakuta watuhumiwa kwenye gari lenye namba za usajili
T.435DHT Costa ya kutoka Madaba kwenda Songea
No comments:
Post a Comment