Thursday, February 9, 2012

AELEZEA SIRI YA KURUDISHA WABUNGE WOTE KATIKA MAJIMBO YOTE CCM MKOANI RUVUMA KATIBU WA CCM

 Katibu  wa CCM mkoani Ruvuma Bw.Emmanuel Mteming'ombe akiweka kitabu cha wageni baada ya kusaini kwenye ofisi za Tujifunze Jana ( Picha na Juma Nyumayo Mhariri msaidizi )
 Bwana Mtemingombe mwenye suti akiwa na mkuu wa kituo kanda ya kusini Bwana Christian Sikapundwa mwenye suluali nyeusi kwenye mlango wa kituo hicho hapo jana ( picha na Juma Nyumayo )



Wananchi wasijiingize kwenye siasa na uwana – Harakati wajishughulishe na kazi zao- Mteming’ombe

WANANCHI wametakiwa kuacha kujishughulisha na masuala ya Kisiasa na kuwa wana harakati  zaidi kuliko kufanya shughuli zao za kuwaletea maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.
Katibu  wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Mkoani Ruvuma Bwana Emmanuel.Mteming’ombe amesema kuwa kila mtu anakuwa mwanasiasa,jambo ambalo linalifanya taifa linakuwa la wanasiasa.na wanaharakati ‘ nawaomba wananchi kuwa kazi ya siasa wawaachie wanasiasa  na wanaharakati wenyewe ,maana ndiyo kazi yao,na wananchi wafanye kazi zao za kujiongezea kipato. Maana kila mtu sasa amekuwa mwanasiasa na mwanaharakati jambo amablo haliwaletei tija’ Alisema Katibu huyo.

Katibu  huyo wa CCM Mkoani Ruvuma ambeye kutokana na mshikamano wa uongozi wa mkoa wa chama hicho,ameweza kurudisha wabunge wa majimbo yote,bila ya kupoteza hata mmoja kwenda chama cha upinzani.

Aidha kati ya wabungea hao wawili wamekuwa mawaziri,mmoja mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,sio kazi ndogo ya kurudisha wa wabunge kwenye nafasi zao,wa zamani na wapya kwenye Chama Tawala wakati wa ushindani  mkubwa wa vyama vingi,Anastahili kupongezwa Bw.Mteming’ombe kwa kazi kubwa aliyoifanya akiwa kwenye nafasi yake ya ukatibu mkuu katika Chama Cha Mapindizi katika mkoa huo.
Katibu mkuu huyo alisema hayo walipozungumza na Blog ya TIJIFUNZE KUSINI alipokuwa akitembelea kiwanda cha uchapai cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Kanda ya Kusini na   kuona hali ya majengo yalioko ndani ya uwanja wa sabasaba ambayo ni kitega uchumi wa chama hicho mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment