Wednesday, February 22, 2012

LEO SIKU YA MAJIVU DUNIANI KOTE KWA WAUMINI WA ROMAN CATHOLIC,ASKOFU MKUU WA JIMBO LA SONGEA NORBET MTEGA AMEOMBA AMANI ITAWALE

 Askofu wa jimbo kuu la Songea Norbert Mtega akigawa majivu baada ya kuyabariki ili kupaka waumini kichwani kama ishara kuwa binadamu ni mavumbi siku moja atarudi tena kua mavumbi.Ikiwa ni siku ya Jumatano ya majivu,ni kipindi cha mfungo kwa Resma kufanya malipizi ya kutubu dhambi na kujisahihisha pale tulipomkosea Mungu.
 Mhasham  Norbert Mtega akibariki majivu katika ibada ya kupaka majivu katika kanisa la Mtakatifu Matias Mlumba Kalemba mjini Songea leo.
 Askofu Mtega anapakwa majivu na Naibu Askofu
 Askofu Norbert Mtega akiwa na majivu kwenda kuanza kupaka waumini baada ya kumpaka mmoja wa Mapadre wake.Katika mahubiri yake alisema kuwa ni kipindi cha toba,katika roho,watoto,vijana,watu wazima na wazee wafanye toba.
Aidha ametoa wito kwa vijana wa Songea na Nchi nzima kuwa wawe watulivu kunapotokea matukio mabaya,na kwamba wasishindane na vyombo vya dola katika kuchukua sheria mkononi.Pia ameomba serikali kuchukua hatua za haraka pale panapotokea tatizo ,na kwamba kuchelewa kutatua matatizo yanapotokea kwa wananchi kunaleta madhara makubwa.
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 aliyoishi Songea alikuwa hajawahi kuona matukio kama yaliyotokea leo la mapambano kati ya polisi na wananchi mabomu ya machozi na mawe kutoka kwa wananchi.Baba Mtega ameomba ushirikiano wa uongozi wa mkoa na taifa na wananchi ili kuleta amani.

 Waumini wanapaka majivu,Juma tano ya majivu leo katika kanisa kuu la Songea
Waumini wa Roman Catholic Songea wameungana na Waumini wengine duniani katika ibada ya majivu,ikiwa ni mwanzo wa mfungo wa Kwaresma.

No comments:

Post a Comment