Tuesday, February 28, 2012

KUMBUKUMBU ZA MASHUJAA WA KINGONI YALIHAMASIHWA NA UTAMADUNI KAMA HUO

 Kijana Athuman Kenezi alikuwa akicheza ngoma ya kitamaduni,ambapo alivaa mavazi yanayoendana na utamaduni wa mwafrika.Isitoshe alicheza na moto,alikula bila ya kuungua mdomo wake.
i
 Bwana Kenezi akinengua,alijipatia kiasi cha fedha Mkuu wa Mkoa Mhe. Mwambungu ,katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi.Maimuna Tarishi na wageni wengine walimzawadia kwa uchezaji wake.
 Kama unavyoona wandishi wa habari wapigapicha walivyokuwa wakipata picha alipokuwa meza kuu.
 Hiyo tu haitoshi wazee wa Kingoni na ngoma yao ya Ligiu yenye asili ya Zulu Afrika Kusini nao walitumbuiza.
 Pamoja na Yote palikuwa na tiba mbadala dawa za asili pia zilionyeshwa.
 Kioda nacho kilikuwepo katika kutumbuiza sherehe hizo sambasamba na ngoma ya Beta.
Ngoma ya Beta kutoka Lizaboni Manispaa ya Songea iliyoongozwa na mzee Masetus Ponera ,Angelika Gama katibu Mwenyekiti Alana Nditi kikundi cha wachezaji 15.

1 comment:

  1. Hii ni hitoria ya kujifunza wengi sana na ni kumbukumbu sana. Nimefurahi kuona hizo ngoma ingawa hakuna sauti ...Nina swali:- Ni hivi unafahamu maana ya rangi ya hizo nguo walizovaa hao akina babu wa asili ya kiZulu?

    ReplyDelete