Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Said Thabit Mwambungu akiongea na waandishi wanachama wa Ruvuma Press katika ukumbi wa maliasili kuhusu ziara ya Makamu wa Rais Dkt Mhe.Mohamed Gharib Bilal mkoani Ruvuma.
Waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Afisa Habari wa mkoa wa Ruvuma Bwana Kasimba
Kaimu RAS wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Anselim Tarimo akisisitiza jambo.
Meza kuu wakisililiza hoja mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari hao
Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu
MKUU wa mkoa wa Ruvuma
Mheshimiwa Said Thabit Mwambungu amewatangazia wananchi wa mkoa wa Ruvuma
kupitia vyombo vya habari mkoani Ruvuma kuwa
kutakuwa na ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt Mohamed Gharib Bilal siku ya Jumanne.
Mkuu wa mkoa huyo
alisema saa 5.00 asubuhi Makamu
atapokelewa uwanja wa ndege na viongozi wa mkoa,kisha kuelekea Ikulu
ndogo,kisha atatembelea hifadhi ya Taifa ya chakula Ruhuwiko na jioni wataweka
jiwe la msingi ukumbi wa mikutano wa Manispaa, kusalimia wananchi kisha kurudi Ikulu ndogo kwa mapumziko.
Alisema kuwa siku ya pili
ya ziara hiyo Makamu ataondoka kwenda wilaya ya Namtumbo – Likuyu Sekamaganga
hadi kwenye mradi wa URENIUM wa Mkuju na kusomewa taafa ya mradi na kukagua
eneo la mradi huo ,kisha kurudi Songea.
Aidha siku ya Alhamisi
Makamu ataelekea wilaya ya Mbinga ambapo atasomewa taarifa ya wilaya katika
gereza la Kitai ,kukagua miradi kisha kuelekea Ruanda TANCOAL kupata taarifa ya
makaa ya mawe,kisha kurudi Mbinga ambapo atazindua mashine za kuzalisha
umeme.ambapo siku ya ijumaa atafanya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa
UMATI ,hatimaye atarudi uwanja wa ndege Songea na kuagwa na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
No comments:
Post a Comment